Mambo Ambayo Mwanamme Anaangalia Kwa Mwanamke Kabla Ya Kumuoa

Mambo Ambayo Mwanamme Anaangalia Kwa Mwanamke Kabla Ya Kumuoa

Urafiki ni muhimu kwa wanandoa. Na mwanamme anapo tafuta mwanamke wa kuoa, ataangalia kama wanaweza kuwa marafiki wazuri.

Ndoa ni kipindi muhimu sana maishani mwa kila binadamu. Na sio wanawake peke yao wanao kuwa na shaka za kupata mchumba, mbali wanaume vivyo hivyo wana shaka na hii ndiyo sababu kwa nini wako makini sana kuangalia wachumba wanao funga ndoa nao kwani hao ndiyo watakao ishi maisha yao nao. Ni mambo yapi ambayo mwanamme anaangalia kwa mwanamke kabla ya kufunga ndoa naye?

Kabla ya kuingia kwa orodha yetu ya mambo ambayo mwanamme ako makini kuona kwa mwanamke, ni vyema kukumbuka kuwa wanawake hawatulii kama maji ya mtungi na kungoja kutahiniwa tu. Mbali, wao pia wako makini na wanaume wanao ingia kwenye uhusiano nao ili kuhakikisha kuwa wanatimiza mambo wanayo yatafuta kwa mchumba wao na mwanamme ambaye wangependa awe baba ya watoto wao ikiwa wana malengo ya kupata watoto katika siku za usoni.

Mambo ambayo mwanamme anaangalia kwa mwanamke kabla ya kumuoa

kuwa hamasisha wanawake

1.Uaminifu

Kila mtu anataka mchumba mwaminifu ambaye hatatoka nje ya ndoa ama uhusiano wao. Ndoa ni kati ya watu wawili walio komaa na walio fanya uamuzi wa kuishi maisha pamoja kwa mema na mabaya. Ili kufanya hivi kwa mafanikio, lazima wawili hawa wawe waaminifu.

2. Urafiki

Urafiki ni muhimu kwa wanandoa. Na mwanamme anapo tafuta mwanamke wa kuoa, ataangalia kama wanaweza kuwa marafiki wazuri. Umuhimu wa kuwa marafiki kwanza kabla ya kufunga ndoa ni kuwa mtakuwa huru kuzungumza kuhusu mambo tofauti maishani hata baada ya kufunga ndoa.

3. Anaye elewa

Hakuna mtu anaye penda kuhukumiwa baada ya kufanya jambo ambalo huenda likawa lilienda mrama tofauti na ulivyo kusudia. Unataka kuwa na mchumba utakaye mweleza ulicho kifanya, unacho kifanya na kwa nini unakifanya.

4. Anaye tunza

nigerian food timetable for adults

Umuhimu wa kuwa na mchumba anaye kutunza ni kuwa hata siku za usoni mnapo amua kuwa wazazi, atawatunza watoto wako. Lakini ikiwa mngependa kubaki bila watoto, mchumba wako atazidi kukutunza.

5. Aliye komaa

Kuna tofauti kubwa sana kati ya uamuzi ulio fanywa na mtu ambaye hajakomaa na aliye komaa. Katika ndoa, lazima uwe umekomaa kwa uamuzi utakao stahili kufanya sio wa mtu mmoja, na lazima uamuzi huo uangalie nyanja tofauti. Kwa hivyo, mwanamme ata tafuta mwanamke aliye komaa ili kuwa naye.

Soma PiaSababu Kwa Nini Uhusiano Wako Haudumu: Jinsi Ya Kuwa Na Uhusiano Unao Dumu

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio