Wazazi wapya hasa wa mara ya kwanza huwa na maswali mengi kuhusu watoto wadogo na safari hii mpya ya ulezi. Tuna angazia mambo usiyofahamu kuhusu watoto wachanga, ili kuwapa maarifa kuhusu mambo ya kutarajia kuona katika watoto wao yaliyo ya kawaida.
Mambo usiyofahamu kuhusu watoto wachanga

1.Watoto hulia bila machozi
Baada ya watoto kuzaliwa, wao huanzia kulia kati ya wiki 2-3 lakini bila kutoa machozi. Katika miezi ya kwanza michache, watoto husumbua sana hasa masaa ya jioni. Mtoto husumbua zaidi katika wiki ya 6 na ya 8.
2. Choo cha mtoto hakinuki
Choo cha mtoto mchanga huwa na ute na maji maji kutoka tumboni na chochote ambacho mtoto amekula tangu kuzaliwa na hakina harufu. Harufu kwenye choo cha mtoto husababishwa na bakteria zinazoenea tumboni. Choo cha kwanza cha mtoto huwa cha rangi ya kijani kisha kubadilika na kuwa kinjano kisha hudhurungi.
3. Alama zingine za kuzaliwa hupotea
Watoto wachanga huwa na alama nyingi za kuzaliwa. Nyingi ambazo huendelea kufifia japo wanapoendelea kukua.
4. Tonsils huwa na tezi za kujua ladha ya chakula
Mtoto mdogo huwa na tezi zinazoweza kujua ladha ya chakula na huwa sawa na zile katika vijana wadogo. Tezi kwenye watoto wachanga huwa zimekuchua sehemu kubwa hadi kufika kwenye upande wa nyuma wa koo. Tezi hizi zinamsaidia kubainisha kati ya vitu vitamu, vitu chachu na vichungu.

5. Watoto wa kiume husimamisha uume wao
Mara nyingi hufanyika mtoto anapotaka kuenda haja ndogo. Unapombadilisha diaper, utaweza kuona. Mama anapofanyiwa ultrasound akiwa na mimba, jambo hili huonekana pia. Sio jambo la kutia shaka kwani ni kawaida.
6. Hulala mara nyingi kwa upande wa kulia
Asilimia 15 ya watoto wachanga wanapenda kuelekeza uso wao kwenye upande wa kushoto wanapolala kwa mgongo. Kupendelea kulala kwa upande huu huchukua miezi kabla ya kutokomea. Kuchagua kulala kwa upande wa kulia kunaweza kutumika kueleza kwa nini watu zaidi wanatumia mkono wa kulia ikilinganishwa na wa kushoto.
7. Kiwango kikubwa cha seli za ubongo
Ubongo wa mtoto mchanga huwa na seli nyingi na idadi ya seli hizi zitaongezeka kwa mara mbili katika mwaka wa kwanza. Una seli za neva nyingi ikilinganishwa na za mtu mkubwa. Hata hivyo seli hizi hufa, watu wazima wana seli za neva chache ikilinganishwa na walivyokuwa wakiwa wachanga.
Soma Pia:Kwa Nini Watoto Wachanga Hulia? Sababu 5 Kuu Zinazowafanya Watoto Wachanga Kulia