Mambo Muhimu Ya Kufanya Baada Ya Tendo La Ndoa!

Mambo Muhimu Ya Kufanya Baada Ya Tendo La Ndoa!

Kukunywa sharubati ya cranberry inapunguza nafasi zako za kupata UTI baada ya ngono. Inasaidia kupigana dhidi ya bakteria.

Je, unafanya nini baada ya tendo la ndoa? Mnakumbatiana kwa muda? Ama unageuka, kutazama upande tofauti na kulala? Ama una enda bafu? Tuna angazia zaidi kwa tunayo yafanya wakati wa kitendo hicho, lakini sio kwa tunayo faa kufanya baada ya ngono.

Lakini, tunacho kifanya baada ya tendo la ndoa ni muhimu sana - na hatuzungumzi kuhusu kukumbatiana hapa tu. Mnayo yafanya baada ya kuwa na kipindi cha kufanya mapenzi kina athari kubwa kwa afya yako.

Kwa hivyo, ni kipi unastahili kufanya dakika chache baada ya kitendo cha wanandoa? Tuna majibu kadhaa, tazama!

Mambo 5 ya kufanya baada ya tendo la ndoa

tendo la ndoa

Ili kuhakikisha kuwa mfumo wa afya ya uzalishaji iko 10/10, una paswa kufuata hatua hizi muhimu.

  1. Enda haja ndogo mnapo maliza

Kukojoa baada ya tendo la wanandoa kunaweza walinda wanawake dhidi ya kupata maambukizi ya kingono ama UTI. Kulingana na daktari wa mambo yanayo husika na mkojo huko mtaa wa New York, David Kaufman, wanawake wanapo enda haja ndogo baada ya kitendo hiki wana toa bakteria ambazo huenda zikawa zimeingia kwa uke wao.

Kwa hivyo kuenda msalani baadaye kuna punguza nafasi zao za kupata UTI. Pia ana shauri unywe maji mengi baada ya kitendo hicho.

2. Jipanguze vizuri

tendo la ndoa

Inasaidia pia unapo jipanguza vizuri. Unapo jipanguza uke wako baada ya kitendo hiki, epuka kutumia sabuni zenye harufu na bidhaa za kusafisha uke. Badala yake, tumia maji ya vuguvugu na sabuni isiyo na harufu kujisafisha huko chini. Una shauriwa kuepuka kutumia vaginal douching. Huenda ukaanza kuhisi hauna starehe, kufura ama kuhisi uchungu wakati wa kufanya mapenzi.

Ukimaliza kujisafisha, jipanguze vyema kutumia taulo iliyo kauka kisha urudi kitandani.

3. Angalia ishara za kutoa damu ama kuhisi uchungu

Unaujua mwili wako vyema zaidi, kwa hivyo usipuuze kitu chochote. Angalia ikiwa una toa damu ama kuhisi aina yoyote ya uchungu. Mtaalum wa rutuba huko New York, daktari Sheeva Talebian anashauri, usi puuze kutoa damu baada a kitendo hiki, huenda ikawa ni ishara kuwa umejeruhiwa ama una maambukizi.

4. Kunywa sharubati ya cranberry

Kukunywa sharubati ya cranberry inapunguza nafasi zako za kupata UTI baada ya ngono. Inasaidia kupigana dhidi ya bakteria. Utafiti pia unadhibitisha kuwa, kunywa glasi ya sharubati ya cranberry kila siku, inasaidia kupunguza ishara za maambukizi ya ngono hadi asilimia 40 kwa wanawake.

5. Tazama kondomu

Una maarifa kwa kutumia kondomu, lakini ni vyema kuwa na maarifa zaidi na kuangalia ilivyo baada ya kitendo chenu. Ili kuhakikisha kuwa haija vunjika. Ikiwa ilivunjika, kuna uwezekano wa kupata maambukizi ya kingono ama kupata mimba.

Kwa hivyo, kumbuka kufuata hatua hizi muhimu baada ya kitendo cha ndoa ili kuhakikisha una linda afya yako!

Soma Pia:Faida Za Kiafya Za Tendo La Ndoa Kwa Wanandoa

Written by

Risper Nyakio