Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

Kuhakikisha kuwa umekula vya kutosha kabla kuenda kufanya mazoezi ni muhimu sana ili kupata mwili unao tamani.

Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yetu. Watu tofauti huanza kufanya mazoezi kwa sababu na malengo tofauti. Huku wengine wakitaka kupunguza uzani zaidi na kuwa na afya nzuri ya kifizikia, wengine wangetaka kuwa na afya bora ya kiakili. Mbali na kufanya mazoezi, ni vyema kwako kufanya mambo ya kufanya kabla ya kufanya mazoezi ili kuhakikisha kuwa unafuzu katika lengo lako.

Tazama orodha hii ya mambo  ya kufanya kabla ya kufanya mazoezi

couple exercises

  • Hakikisha umelala vya kutosha

Mwili wako unapumzika vya kutosha unapo lala. Mwili wako unaanza kupona unapo lala. Usingizi wa kutosha na bora ni muhimu ili upate nishati tosha ya kufanya kazi zako na kufanya mazoezi pia.

  • Kula vizuri

Kuhakikisha kuwa umekula vya kutosha kabla kuenda kufanya mazoezi ni muhimu sana ili kupata mwili unao tamani. Unashauriwa kuhakikisha kuwa umekula angalau lisaa limoja ama mawili kabla ya kufanya mazoezi, ikiwa unafanya mazoezi yako jioni. Kwa wanaopenda kufanya mazoezi asubuhi, hakikisha umekula ndizi ama tufaha ili upate nishati tosha ya kufanya mazoezi. Pia, unataka kuhakikisha kuwa nishati yako inatoka kwa chakula na sio kwa misuli yako. Kwani ikiwa inatoka kwa misuli, huenda ukakosa kutimiza lengo lako la mwili wa ndoto zako.

  • Kunywa maji mengi

Maji ni muhimu sana kwa utendaji kazi wa mwili wako wa kawaida. Ni muhimu kuhakikisha kuwa unakunywa maji tosha kwani utatoa jasho jingi unapo fanya mazoezi. Kutoa jasho kuna maana kuwa mwili wako unapoteza maji, ambayo unahitajika kuyarejesha. Maji pia yana kusaidia kuwa na viwango vya juu vya nishati unapo fanya mazoezi yako ya kila siku.

  • Kunyoosha mwili

Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

Hili ni jambo muhimu sana hata ingawa watu wengi hupuuza faida zake. Kunyoosha kunasaidia kulegeza mwili wako uwe tayari kufanya mazoezi. Pia, ubora wa mazoezi utakayo yafanya utalingana na kama ulinyoosha mwili wako kabla ya kuanza mazoezi yako ama la.

Hitimisho

Mazoezi ni muhimu sana, na pia kuyafanya kwa njia inayo stahili. Vidokezo vyetu vinakusaidia kuhakikisha kuwa umejitayarisha inavyofaa kabla ya kuanza kuyafanya. Hakikisha umevalia mavazi ya mazoezi na viatu vinavyo faa ili kuepuka kuto kuwa na starehe katika mazoezi yako, ama kuumia miguu.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Lishe Na Mazoezi Haya Yatakusaidia Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Written by

Risper Nyakio