Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Homa Ya Corona Na Ujauzito

Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Homa Ya Corona Na Ujauzito

Mama mjamzito kwa wakati mwingi huwa na mawazo tele, kana kwamba haya hayatoshi, lazima afikirie kuhusu homa ya corona. Ila ni muhimu sana kwa afya yako na ya mwanao.

Lazima uwe na ujuzi kuhusu, COVID-19 umeenea kote ulimenguni. Hivi karibuni shirika la afya duniani limetambua COVID-19 kama janga. Ingawa umjamzito, unahofu kuhusu madhara ya COVID-19 kwa afya yako; na uhusiano uliopo kati ya homa ya corona na ujauzito. Makala haya yatajibu maswali yako, na pia kumaliza hofu, unapojitayarisha kujifungua.

Homa ya Corona: Kila kitu unachohitajiwa kufahamu

coronavirus and pregnancy

Kama ulivyoskia, homa ya Korona inaenea kupitia matone ya upumuzi yanayotumwa hewani pale ambapo mtu aliyeaathirika na Korona anakohoa au kuchemua. Ugonjwa huu pia unaeza kunea pale ambapo mtu anagusa uso ambao una virusi hivi.

Kwa sababu virusi hivi ni vipya, wataalam wana ujuzi kuhusu madhara ya homa ya corona kwa ujauzito. Wataalam wanasema kwamba wanawake wajawazito wana uwezekano wa kushikwa na dalili za homa hii ya Korona. Ujumbe wa sasa hivi unapendekeza kwamba dalili ni kidogo au wastani; huu pia ndio ukweli kwa wanawake wasio wajawazito na wanaume.

Kulingana na Vituo vya kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC), wanawake wajawazito ambao wanapatwa na mabadiliko mwilini, yanaweza sababisha hatari ya kushikwa na maambukizo. Kuwa na virusi vya familia moja  kama COVID-19 na maambukizo mengine ya upumuzi, kwa mfano Influenza, wanawake wamekuwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na magonjwa makali. Ni muhimu kujikinga kutokana na magonjwa kama umjamzito.

Je, COVID-19 inaongeza hatari ya kupoteza mimba au shida zingine?

Haionekani kama COVID-19 inasababisha hatari ya kupoteza mimba au shida zingine; Kama vile kasoro ya maumbile kwa wanawake waliopatwa na virusi hivi. Kulingana na data kutoka kwa homa zingine za Korona kama vile SARS na MERS , Chuo cha Elimu Marekani  cha wakunga na wanajikolojia wanaona kwamba kina mama wajawazito ambao wanapatwa na COVID-19  wanakuwa na uwezo mkubwa wa kupatwa na shida, kama vile kujifungua kabla ya wakati sawa kufika. Lakini ujumbe huu ni mdogo na maambukizi hayawezi kuwa kamili ndio sababisho la tatizo hili.

Homa ya Corona na Ujauzito: Je, ikiawa umeathirika unaeza kuueneza kwa kiinitete?

homa ya corona na ujauzito

Kuna utafiti wa wanawake tisa wajawazito ambao walikuwa na COVID-19 na walikuwa na dalili hizi. Utafiti huu ulionyesha kwamba watoto hawakushikwa na homa hii. Virusi hivi havikupatikana katika ugiligili wa uzazi, koo za watoto hawa au katika maziwa ya uzazi. Hatari ya kueneza maambukizo haya kwa fetusi inaonekana kuwa katika kiwango cha chini, pia hakuna ushahidi wa kuonyesha shida za maumbile katika mtoto au madhara mengine kutokana na maambikizi ya uzazi ya COVID-19.

Ingawa utapatwa na Homa ya corona baada ya kujifungua, hakuna ushuhuda wa virusi hivi katika maziwa ya mtoto. Kwa sababu virusi hivi vinaenea kupitia matone ya upumuzi, unafaa kuosha mikono yako na kuvaa barakoa ili kupunguza athari ya kueneza virusi hivi kwa mtoto.

Nini itafanyika katika sherehe za kukaribisha mtoto?

Sherehe hii ni muhimu na ni ya furaha sana, wakuu wa afya wamependekeza umbali wa kutangamana kwa watu ili kupunguza kueneza virusi hivi.  Sana sana katika mikusanyyiko ya watu, hatari ya kushikwa na maambukizi haya iko katika kiwango cha juu. Ni muhimu sana kupunguza kukusanya na watu kwa wakati huu. Pia, tafadhali epukana na kutembea katika maeneo mbali mbali. Wataalam wana hofu kwamba virusi hivi vimeenea kote na nchi kadhaa zimefunga maboda yao.

Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi hivi wakati ya ujauzito

homa ya corona na ujauzito

Jambo la muhimu sana ni kuzingatia usafi kwa kunawa mikono kutumia sabuni na maji kwa sekunde 20.

 • Epuka na kugusa macho, mdomo na mapua yako.
 • Unafaa pia kuepuka mkusanyo wa watu. Umbali wa muingiliano kunasaidia kupunguza kuenea kwa virusi hivi.
 • Kama umeathirika na mafua au kukohoa, kaa nyumbani ili upunguze kueneza kwa watu wengine. Hii ni kumaanisha hakuna kwenda kanisani au sokoni.
 • Kuchemua na kukohoa katika karatasi shashi ambayo utatupa, katika kiwiko chako, ili kuzuia watu wengine kugonjeka.
 • Kunywa maji na kuwa na wakati wa kutosha wa kupumzika pia inasaidia kuimarisha mfumo wako wa kinga.
 • Tembelea daktari kwa huduma za ujauzito. Hakikisha kwamba umeongea na daktari wako ili muwe na uelewano sawa.
 • Jikinge kutokana na mtu ambaye ana dalili za ugonjwa huu. Dalili hizi ni kama vile joto mwilini na kukohoa sana.
 • Jikinge na kutumia usafiri wa umma, hakikisha kwamba unasafiri wakati ambapo hakuna trafiki.
 • Fanyia kazi nyumbani, iwezekanapo. Mwajiri wako anapaswa kukushauri kuchukua hatua hii.
 • Epuka mkusanyiko na marafikiu na familia. Wasiliana nao kupitia simu na mtandao wa kijamii.
 • Jikinge kutokana na mikusanyiko mikubwa na mikusanyiko midogo katika maenea ya umma kama vile pabu, sinema, mikahawa, baa na klabu.
 • Tumia simu yako na huduma za mtandaoni ili kuwasiliana na daktari wako.

Harvard Health   CDC   BBC

Soma pia: 11 Common Terms And Phrases Wen Yu Suppose Sabi About Coronavirus Disease

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio