Rutuba ya kiume haitazamiwi kama jambo kubwa hadi pale ambapo wanandoa wanachukua muda mrefu kutunga mimba. Hata kama ni baada ya mama kufanyiwa kipimo. Kuna mambo yanayo athiri uzalishaji wa kiume ambayo wanaume wanastahili kuangazia kama kubadili mitindo yao ya maisha ili kuboresha nafasi zao za kutunga mimba na kupata ushauri kabla ya kutunga mimba.
Kuna baadhi ya shirika zinazo husika na kuwaelimisha wanaume kuhusu afya yao ya uzalishaji. Ikiwa utajaribu kupata watoto, ni vyema kwako kuwa makini na afya yako kwani afya ya manii ni muhimu kwa mtoto. Ni muhimu kwa wanaume kufanya mtindo wa kutembelea vituo vya afya mara kwa mara hata wasipokuwa na fikira za kupata watoto. Wasipo jitunza, wana hatarisha maisha ya mama na mtoto. Watoto ambao baba zao wana matatizo ya kiafya kama kisukari, uzito wa kupindukia na kuvuta sigara, wako katika hatari ya kupata shinikizo la damu.
Mambo matatu yanayo athiri uzalishaji wa kiume
Uzito

Wanaume wengi hawana habari kuwa uzito wao unaweza kuathiri uwezo wa wachumba wao kupata mimba. Kuwa na uzani wa kupindukia kunaweza punguza idadi na mwendo wa manii. Na kumaanisha kuwa mchumba atachukua muda zaidi kushika mimba. Wanaume walio na uzani wa mwili wa kupindukia wana kiwango cha chini cha testosterone na kuathiri uwezo wao wa kuwa na mapenzi mara kwa mara.
Mtindo wa maisha

Mitindo hasi ya maisha kama uvutaji wa sigara, kutumia mihadarati na kula vyakula visivyo na manufaa mwilini. Uvutaji wa sigara unaweza athiri watoto wako. Wanawake wameelimishwa na sio rahisi kupata mjamzito akivuta sigara. Ila, mwanamme anaye vuta sigara anaweza kuathiri mtoto wake ambaye hajazaliwa? Wanaume wanaovuta sigara huwa na nafasi changa za kutunga mimba ikilinganishwa na wanaume wasio vuta sigara. Ni vyema kwa wanaume kupunguza na kisha kuwacha utumiaji wa sigara muda kabla ya kujaribu kupata watoto.
Umri

Ubora na kiwango cha manii hupunguka wanaume wanapotimiza umri wa miaka 45. Na kumaanisha kuwa inachukua muda mrefu zaidi kwao kupata mtoto na kuwa na nafasi za juu kupoteza mimba. Baadhi ya wakati mwanamke anaposhuhudia matatizo katika mimba yake, huenda ikawa chanzo ni mwanamme hata kama yeye ndiye atakaye athiriwa. Wanaume wanafahamu kuwa wanawake wana muda ambao wanatatizika kupata mimba, ila hawafahamu kuwa wao pia wana saa ya kibiolojia.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Njia 5 Za Kuboresha Mfumo Wa Uzazi Katika Wanawake