Wanawake, Tazama Mambo Unayo Yafanya Yanayo Wavutia Wanaume

Wanawake, Tazama Mambo Unayo Yafanya Yanayo Wavutia Wanaume

Wanaume wengi wanapenda michezo kwa hivyo wanafurahia wanapo patana na mwanamke anaye penda angalau mchezo mmoja.

Unapo ingia katika uhusiano na mchumba wako ambaye pia ni rafiki yako mkubwa, utaanza kuangalia mambo ambayo anafanya yanayo kufurahisha. Hata mambo machache yasiyo kaa makubwa kwake, huenda yakafanya wakuvutie zaidi. Je, ni mambo gani yanayo kuvutia zaidi kutoka kwa mchumba wako? Tazama baadhi ya mambo tuliyo orodhesha yanayo wavutia wanaume.

Mambo Yanayo Wavutia Wanaume

Wanawake, Tazama Mambo Unayo Yafanya Yanayo Wavutia Wanaume

  1. Una ndoto na malengo maishani

Tofauti na imani za watu wengi kuwa wanaume wanataka mchumba atakaye baki nyumbani bila kufanya chochote. Unapo kuwa na malengo kamili na dhabiti maishani kisha kufanya juhudi kuyatimiza, unawavutia wanaume kwako. Kwani wanataka kuwa na mchumba ambaye wana saidiana nyumbani.

2. Unapenda kula na kupika

Wanaume wanafurahia wakati ambapo mwanamke anaweza mpikia chakula kizuri na kitamu. Sio lazima uwe mpishi hodari, ila juhudi ndizo muhimu. Na wanaume wanapendelea zaidi unapo weza kula chakula bila kuogopa. Kwani wao pia wanapenda chakula na wana hamu kubwa ya kula.

3. Kuvalia mavazi yake mkiwa nyumbani

Mnapo kuwa kwenye nyumba mmetulia bila kazi yoyote, usi one haya kuvalia mavazi yake. Hata kama wanawake wengi hawa fahamu jambo hili, wanaume wanapendelea kuwaona wachumba wao wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa pamoja kwenye nyumba. Usione haya kuvalia suruali zake mkiwa pamoja.

4. Mwanamke anayependa michezo

Wanawake, Tazama Mambo Unayo Yafanya Yanayo Wavutia Wanaume

Wanaume wengi wanapenda michezo na hata kama sio kadanda, huenda wakawa wanafuata mpira wa vikapu na michezo mingine. Kwa hivyo wanafurahia wanapo patana na mwanamke anaye penda angalau mchezo mmoja. Wanapo enda kutazama wachezaji wakicheza, wanaweza jumuika pamoja.

5. Kucheka pamoja na kufanya mambo ya kufurahisha

Uhusiano unapaswa kuwa wenye furaha, mkiwa na mchumba wako ambaye pia ni rafiki yako. Mchumba wako anapo weza kukufanya ucheke na ufurahie mara kwa mara, anahisi kuwa ametimiza na ujasiri wake unaongezeka.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo wanawake katika uhusiano hufanya yanayo wavutia wanaume. Je, ni mambo yapi yanayo kuvutia kwa mchumba wako? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!

Soma Pia: Mambo 10 Ambayo Mpenzi Wako Wa Kiume Kamwe Hata Sema

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio