Wamama Waongea Kuhusu Mambo Waliyo Ambiwa Walipo Kuwa Na Mimba

Wamama Waongea Kuhusu Mambo Waliyo Ambiwa Walipo Kuwa Na Mimba

Watu wengi huwa wakarimu kwa wanawake wenye mimba. Ila sio kikundi hiki cha watu tunacho angazia.

Watu huwa wakarimu kwa wanawake walio na mimba. Sio jambo geni kwa watu kuwapa viti wakae kwenye gari kwa sababau wana mimba ili wapumzishe miguu yao iliyo choka. Baadhi ya wakati, hata kwenye foleni za benki, wanawake wajawazito mara nyingi wanakubalishwa kuhudumiwa kwanza. Haijalishi jinsi ilivyo ngumu huko nje ama ukali wa watu. Wanawake wenye mimba na wazee mara nyingi huonyeshwa ukarimu na watu wageni. Ila, watu wengine ni tofauti. Hawajali ama hawajui jinsi ya kuwaongelesha kwa ukarimu. Wamama hawa wana tu hadithia baadhi ya vitu walivyo ambiwa walipo kuwa na mimba. Ni sawa kukasirishwa na maneno haya ya kukera.

Angalia baadhi ya maneno haya ya kukera wamama waliambiwa walipo kuwa wajawazito

ridiculous remarks

"Siku moja kazini, mfanyakazi mwenzangu aliniuliza kama hatuna runinga nyumbani. Nilipata mimba tena miezi mitano baada ya kujifungua kifungua mimba changu. Alihisi kuwa kama kungekuwa na runinga nyumbani, hatunge tumia wakati mwingi sana kitandani. Niliitikia kwa kunyongwa na kinywaji changu. Nili tarajia watu waongee kuhusu jambo hilo, kwa hivyo sikuwa na shida." Kemi O. Public Servant, Facebook.

"Nilikuwa kwenye banki siku moja, wakati mzee mmoja aliniangalia na kusema, "hongera mama" kwa sauti ya juu. Kwa kasi nika shangaa, kwa nini. Kwa sababu nilikuwa wiki kumi na mbili katika safari yangu ya ujauzito na bado tumbo haikuwa imeanza kuonekana. Nilipo mwuliza kwa nini, akasema, "mtoto bila shaka!" Kwa kasi nikavutia uangalifu wa kila mtu. Nika mshukuru na kugeuka kwa kero. Hadi dakika hiyo, sikuwahi mfahamu mwanamme huyo." Binta U. Creative Artist, Lagos.

"Watu wachache waliniita 'arugbo' nilipokuwa mjamzito. Nashangaa mbona, kwa sababu 'arugbo' ni jina la ki Yoruba la "mtu mzee". Siku moja, nikauliza mmoja wao kwa nini, kwa sababu nilitaka kuelewa. Akaniambia kuwa baadhi ya wanawake kwa ujumla huonekana wazee wanapo kuwa na mimba. Olufunke O. Banker, WhatsApp.

Maneno ya kukera zaidi

Wamama Waongea Kuhusu Mambo Waliyo Ambiwa Walipo Kuwa Na Mimba

Baadhi ya matamshi haya ya kukera huwa ya watu wanao jaribu kupata ujumbe zaidi kutoka kwako, wanapo enda, "unajifungua siku gani?" "Bado unakula chakula cha watu wawili?" "Tumbo yako ni kubwa, una uhakika hautarajii mapacha?" Nyakati zingine, matamshi huwa na tofauti ndogo sana na matusi, ama imani za kuaminika zisizo za kweli. Watu huwa na kasi ya kutabiri jinsia ya mtoto wako, kwa hivyo wana kwambia kuwa una tarajia kijana wakati ambapo mambo ni magumu kwako, ki-fedha.

Pia wanakwambia kuwa ni msichana wakati ambapo haupendezi sana na uso wako umefura kufuatia ujauzito. Wata kwambia kuwa amechukua urembo wako wote.

Walio wabaya zaidi ni wageni ambao wanajua ni kipi kinacho kufaa kuliko daktari wako aliye na historia yako ya kimatibabu ya maisha yako yote.

"Nilikuwa naendesha karibu na duka na kuamua kununua chupa ya maji kwa sababu nilikuwa na kiu. Mwanamke huyo mzee dukani ali angalia tumbo yangu na kuniambia kwa ukali kuwa hakuwa ananiuzia kinywaji baridi. Badala yake alinipa chupa ya maji na kunifukuza." Opeyemi A. Realtor. Facebook

Mwishowe, ni wanafamilia wanao kulinda zaidi ndio wa mwisho kwenye meza hii. Kama mama anaye mpigia bintiye aliye na mimba kila jioni, kuhakikisha kuwa amefika nyumbani kabla ya saa kumi na mbili jioni. Kwa sababu "wanawake wenye mimba hawapaswi kukaa nje baada ya saa kumi na mbili za jioni."

How To Handle It

maneno ya kukera kwa wajawazito

Kwa kutumia maneno ya Michele Obama hapa. Wakienda chini na maneno yao ya kukera, wewe mama mrembo uliye na mimba unaweza enda juu. Wacha wabaki wakiongea wakiwa chini yako. Mambo muhimu ni kula vyakula vyenye afya, kujitunza ili kutunza mwanao na kuifurahia safari yako ya mimba hadi pale ambapo utajifungua. Na usisahau kupendeza hata unapo kuwa na mimba.

Ni kipi ambacho mtu aliwahi kukwambia ulipo kuwa mjamzito na hadi wa leo hujai amini? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini.

Soma pia: Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

Written by

Risper Nyakio