Hizi Ndizo Sababu Mtoto Wako Anahitaji Mtama

Hizi Ndizo Sababu Mtoto Wako Anahitaji Mtama

Guinea Corn has several health benefits for babies. It is advised that you breastfeed your baby exclusively for six months and introduce weaning foods after.

Mtama ambao pia hujulikana kama wimbi ni chakula kinachoongeza nguvu mwilini. Hii ni kwa sababu ina mirabaraba na protini. Mtama hutoa baadhi ya protini, vitamini na madini yaliyo na umuhimu kwa ukuzi na ustawi wa mwanadamu. Tutaangazia manufaa ya kiafya ya mtama  kwa wototo wachanga.

lishe ya mtama

Chakula hiki kikubwa kina wingi wa madini kama vile vitamini B, nahasi, ironi, potasiamu,magnesi  na kadhalika. Haina faida za kiafya kwa watu wazima peke yao mbali pia kwa watoto haswa. Hili zao kuu ni nafaka iliyotokana Africa.  Watu huila duniani nzima.  Ina thamani haswa maeneo yaliyo kame kwani ina ukinzani mkubwa kwa kiangazi.  wimbi ni nafaka iliyojaa madini na mara nyingi husagwa kuwa  unga.  Watu hutumia hii nafaka kutengeza mikate, uji na chapati za maji.

Manufaa ya mtama

mtama wa mtoto

Wimbi  hujulikana kama chakula kinachoongeza nguvu mwilini kwa sabubu kina wingi wa protini,mirabaraba  na madini mengine kama vile:

 • Ironi
 • Vitamini b
 • Nahasi
 • Kalisiamu
 • Potasiamu

Hii nafaka ya ajabu, ni asili muhimu ya tannins na three - deoxy anthocyanidins.  Hizi hugandamiza kukua kwa seli za saratani ya koloni.

Faida za kiafya za mtama

chakula bora cha mtama

Kina mama wengi nchini Nigeria wamegeukia mtama kama chakula cha kwanza kigumu cha kumpa mtoto. Kuna sababu nyingi kwa nini unafaa kuongeza mtama katika chakula cha mtoto wako. Na hapa ni mojawapo wa hizo sababu:

 1. Zile protini na vitamini ambazo hupatikana kwenye wimbi ni nzuri kwa watoto kama zilivyo kwa watu wazima. Kama chumba kizima cha lishe bora, mtama una kila kitu kinachohitajika kuyatosheleza mahitaji ya kiafya ya mtoto wako.
 2. Watoto walio na uzani wa chini mara nyingi huchelewa kukua kimwili na kisaikolojia. Iwapo mtoto wako ana shida kuongeza uzito anzisha hiki chakula katika lishe yao. Kula wimbi peke yake au kama kunu Geida itamwezesha mtoto wako kupiga hatua kubwa haraka.
 3. Hukomaza mfumo wa kuyeyusha chakula. Kwa hivyo kwa usaidizi wake unaweza epukana na matatizo mengi ya mmengenyo.
 4. Huzuia saratani. Mtama una utajiri wa three-deoxy anthocyanidins na tannins. Hizi kampaundi za phenolic huzuia kukua kwa seli za saratani za koloni na za matiti.
 5. Wimbi humsaidia mtoto kuongeza uzani.  Kina Mama kwa mara nyingi hutatizika na hali ya afya ya watoto wake na hufanya kila jitahada kuibadiilisha. Njia mojawapo iliyo nzuri na yenye ufanisi mkubwa ni kuongeza ulaji wa kalori.
 6. Hiki chakula kina wingi wa protini, mafuta na wanga ambazo uhitajika katika kukua kwa mtoto.
 7. Mtama ni mojawaopo wa vyanzo bora vya protini. Huwa pia na vitamin nyingi. Huwa na umuhimu kwa afya ya mtoto.

Sasa wajua faida za kiafya za mtama, unaweza kumpa mtoto wako kuboresha afya yake. Ijaribu!

Guardian NG

Also read: Baby Food Recipes For Your 9-Month-Old

Written by

Risper Nyakio