Haya ni majibu machache yanayo sikika mwanamke anapo chagua kuwa angependa kujifungua kwa njia asili kupitia kwa uke.. dawa za uchungu na kujifungua kusiko ingiliwa kati. Kujifungua kwa njia asili huwa uamuzi mgumu kwa mwanamke yeyote kufanya na badala ya kupongezwa kwa kupitia uchungu mwingi bila usaidizi, wana laumiwa kwa uchaguzi walio ufanya. "Hakuna zawadi..." huenda ikawa ni mojawapo ya majibu yanayo vunja moyo zaidi kwani wanawake wanao pitia uchungu huu huhisi kana kwamba kuna tuzo baadaye. Huenda ikawa sio tuzo ya kifizikia lakini ya kiakili. Yeeei! Umefaulu kufanya hivi! Kujifungua kwa njia asili sio kwa kila mtu na kuna wanawake wasio na uamuzi katika jambo hili. Wakati ambapo hakuna tuzo kwa wanawake wanao jifungua kwa njia asili, kuna hatari kwa wanawake wanao tumia usaidizi wa kimatibabu kujifungua. Tazama manufaa ya kujifungua kwa njia asili.
Baadhi ya manufaa ya kujifungua kwa njia asili

Hii ni mojawapo ya mbinu za kuingilia kati zinazotumika mwanamke anapo jifungua kupitia kwa uke. Wanawake wengi hawana uamuzi wowote katika suala hili. Vitu kama shinikizo la juu la damu, fetal distress na kadhalika vinahitaji induction kwa usalama wa mama na mtoto. Kuna wakati ambapo sio lazima tendo hili kufanyika. Kama vile mtoto anapo chelewa kuzaliwa. Walakini, siku anayo tarajiwa, ndiyo inayo tumika kudhibitisha. Watoto wengi huenda wakawa, bado hawako tayari kutoka tumboni mwa mama siku wanayo tarajiwa. Ikiwa mama na mtoto hawa yuko tayari kwa uchungu wa uzazi, huenda matatizo yaka ibuka kwa urahisi. Wanawake wengi wameambiwa kuwa induction inahitajika kwa sababu ya kuwa na mtoto mkubwa, ila baadaye wakajifungua mtoto mdogo kuliko alivyo tarajiwa. Inductions zinaweza sababisha matumizi ya dawa za uchungu zisizo hitajika, matumizi ya forceps ama C-section katika kesi zingine. kujifungua kwa njia asili kunaweza sababisha hitimisho kama hizi, lakini kwa nafasi changa zaidi.
Katika vitabu vya ujauzito, maji ya mama yana paswa kuvuja punde tu baada ya uchungu wa uzazi kuanza na kuharakisha mchakato huo. Baadhi ya wakati ama wakati mwingi, vitu havifuati ilivyo vitabuni. Daktari anaweza vuja gunia la maji la mama kwa sababu moja ama mbili, mara nyingi; kuanzisha uchungu wa uzazi ama kuongeza spidi ya mchakato huo. Daktari anapo fanya hivi, matatizo yanaweza ibuka. Huenda mambo yaka enda inavyo kusudiwa ama C-section ikahitajika. Hii ni kwa sababu, baada ya maji kuvuja, mwanamke hana wakati mwingi wa kujifungua kabla ya hatari ya maambukizi kuongezeka. Madaktari kwa ujumla humpa wakati fulani baada ya maji kuvuja kabla ya upasuaji kufanyika. Wanawake wengi huvunjwa maji bila matatizo yoyote, lakini kama hakuna umuhimu kwa mama na mtoto mwenye afya, ni vyema kuwacha vitu vitendeke kwa wakati wake.

Kwa wanawake wengi, epidural huwa chaguo bora kwa kujifungua kwao. Epidurals ni nzuri kwa mwanamke aliye kuwa kwa uchungu wa uzazi kwa muda mrefu na anahitaji kupumzika ili kuendelea. Pia, epidural inaweza mtuliza mama kwa kuharakisha uchungu wa uzazi katika visa vingi na mama aliye tulia.
Walakini, njia hii ya kujifungua huja na malipo ya juu. Shaka kubwa zaidi ya wanawake wengi wanao taka epidural ni uwoga wa C-section. Hata kama hakuna udhabiti hasa kuwa baada ya epidural njia ya kujifungua ya kipekee itakuwa c-section, kuna hofu nyingi kati ya wanawake wanao chagua njia hii. Na pia kuna hatari zingine zinazo husika na epidural ambazo haziko na kujifungua kwa njia asili.
Wakati ambapo epidural ndiyo matibabu yanayo julikana zaidi kwa uchungu wa uzazi usio starehesha, kuna mbinu zingine kwa wamama walio katika uchungu wa uzazi. Kama vile narcotic, nitrous oxide, pudendal block, spinal tap, dawa za kupunguza uchungu na kadhalika. Hii si kusema kuwa vitu haviendi mrama na kujifungua kwa asili kwa sababu bila shaka vinaweza. Walakini, kadri unavyo zidi kuenda mbali na kujifungua kwa njia asili, ndivyo unavyo zidi kuwa katika hatari ya kitu kuenda mrama.
Hitimisho
Kila mwanamke ni tofauti na uchungu wa uzazi huwa tofauti kwa kila mmoja. Kuna manufaa mengi ya kujifungua kwa njia asili. Kujua kuwa mwanao alizaliwa bila usaidizi wowote. Sio kusema kuwa kuna ubaya wa kujifungua kupitia kwa mbinu yoyote ile, huenda baadhi ya wakati, mwanamke hana usemi katika kujifungua kupitia kwa c-section. Cha maana zaidi ni kujifungua mtoto salama na maisha ya mama na mtoto kuwa salama.
Soma pia:Yote Unayo Hitaji Kufahamu Kuhusu Dhiki Baada Ya Kujifungua