Uyoga ni aina ya kuvu iliyo salama kuliwa na binadamu. Hata ingawa ina manufaa mengi ya kiafya, ulaji wake bado hauja kumbatiwa inavyo paswa na watu hasa kutoka nchi za Kiafrika. Uyoga ni aina ya mboga inayo paswa kununuliwa mara zaidi unapo fanya ununuzi wa vyakula vyako vya nyumbani. Soma manufaa ya kula uyoga.
Manufaa ya kula uyoga

- Ni vyanzo vya vitamini D
Ni vigumu kupata vitamini D kwa vyakula, ila uyoga una wingi wa vitamini ya aina hii. Unapo fichuliwa kwa mwangaza, uyoga una uwezo wa kutengeneza vitamini D. Aina tofauti za uyoga kama white buttons zinazo iga vifungo, portabella, na brown cremini.
2. Ladha sawa na nyama
Kwa watu ambao hawapendi nyama, wanao pata matatizo ya kiafya wanapo kula nyama na wanao ishi maisha bila ulaji wa protini kutokana na wanyama (vegans), uyoga ni anuwai bora. Ina sawa ladha na nyama na ina wingi wa protini kwa hivyo ni mbadala mwema wa nyama.
3. Zina wingi wa selenium
Selenium ina fanya kazi sawa na anti oxidants mwilini na kulinda seli dhidi ya hatari yoyote ambayo inaweza sababisha magonjwa. Pia ina jukumu muhimu katika mfumo wako wa kinga.
4. Zina fanya kazi sawa na nyama kwenye chakula
Unapo tayarisha chakula kinacho hitaji nyama ya aina yoyote ile, tumia uyoga kama mbadala wa nyama. Kwa kufanya hivi, utapunguza idadi ya kalori na ufuta unazo tia mwilini.
5. Kupunguza uzani wa mwili

Uyoga una viwango vidogo sana vya kalori. Katika chakula cha white buttons tano, kuna kalori kama 20. Na bado utahisi kushiba sana. Kwa wanao kula uyoga kama chamcha chao badala yao wana punguza idadi ya kalori wanazo tia mwilini na kuhisi shibe sawa na aliye kula nyama.
6. Ni rahisi kukuza
Uyoga hauhitaji vitu vingi kukuza. Unaweza kuza ndani ya nyumba ama hata nje ya nyumba kwa urahisi. Na unapo kula uyoga, una punguza kiwango cha carbon unacho weka mwilini.
Hitimisho
Ikiwa unataka kuishi maisha bora yenye afya na kupunguza idadi ya kalori unazo kula. Hakikisha kuwa una nunua uyoga zaidi na kuwapikia wanajamii wako. Ikiwa unafurahia kula uyoga, tujulishe jinsi unavyo penda kutayarisha uyoga wako!
Soma Pia: Keto Kwa Watoto: Je, Lishe Ya Keto Ni Salama Kwa Watoto?