Kunyonyesha huwa na manufaa mengi kwa wote mama na mwanawe. Je, unafahamu manufaa ya kunyonyesha? Mama aliyejifungua anahimizwa kunyonyesha kwa kipekee kwa miezi sita. Ambapo hamlishi mtoto kitu chochote mbali na maziwa ya mama.
Manufaa ya kunyonya kwa mtoto mchanga

Maziwa ya mama ni lishe bora kwa mtoto mchanga kwani yana virutubisho vyote vinavyohitajika katika ukuaji bora wa mtoto. Na kudumisha ukuaji na maendeleo yake hadi anapofikisha miezi sita ya umri. Maziwa ya mama ni rahisi kumeng'nywa na kutumika mwilini kwa urahisi. Maziwa haya yana kingamwili na uwezo wa kumlinda mtoto kutokana na maambukizi, kuharisha ama ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini.
Manufaa ya kunyonyesha kwa mama
- Maziwa ya mama ni bure, ikilinganishwa na maziwa ya kopo ama ya formula ambayo yana bei ghali.
- Yanapatikana kwa urahisi na wakati wowote mtoto anapojihisi kunyonya
- Kunyonyesha kunamsaidia mama kupunguza uzani wa mwili
- Kunyonyesha kwa kipekee kuna saidia kuepusha dhidi ya mimba
Unyonyeshaji wa kipekee

Unyonyeshaji wa kipekee unashauriwa kwa watoto walio na chini ya umi wa miezi sita. Unyonyeshaji wa kipekee ni pale ambapo mama anamlisha mtoto maziwa ya mama bila kuongeza chakula kingine. Mama anapojihusisha katika tendo la ndoa bila kinga na huku hanyonyeshi vya kipekee, ako katika hatari ya kupata mimba angali ananyonyesha mtoto mwingine.
Kulinganisha umuhimu wa kunyonyesha kati ya mama na mtoto
Mama |
Mtoto Mchanga |
Ni rahisi kupatikana |
Ina virutubisho vyote muhimu |
Ni bei rahisi ikilinganishwa na maziwa ya kopo |
Mtoto anaweza kufyonza na kumeng'enya kwa urahisi |
Mama anahisi kuridhika anaponyonyesha |
Yana joto inayohitajika |
Hupunguza uvunjaji wa damu |
Ni safi na tayari kunywiwa |
Husaidia kupunguza uzani baada ya kujifungua |
Ina kingamwili muhimu kuepusha maambukizi |
Hudumisha upamoja kati ya mama na mtoto |
Humlinda mtoto dhidi ya mzio |
|
Kuzuia mtoto dhidi ya kuharisha |
Maziwa ya mama ni salama kwa mtoto, mama hahitaji kuongeza chochote kabla ya kumlisha mwanawe na ni bora kwa afya yake. Yana virutubisho vyote hitajika kwa pamoja na mama hana shaka kuwa mtoto atakosa chochote.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Jinsi Ya Kunyonyesha Mtoto Na Umuhimu Wa Kumshika Mtoto Ifaavyo