Kutopata usingizi tosha kumehusishwa na matokeo hasi ya kiafya. Kulingana na Kituo cha Kulinda na Kuepusha dhidi ya Maradhi (CDC), moja kati ya watu watatu hawapati usingizi tosha. Jambo linalowafanya watu wengi kutafuta suluhu la kinyumbani la tatizo hili ili kuwawezesha kulala vyema. Kunywa glasi ya maziwa kabla ya kulala ni kitendo maarufu kinachosaidia kukupumzisha, kutoa wasiwasi na kukusaidia kulala vyema usiku. Je, unafahamu manufaa ya kunywa maziwa kabla ya kulala? Tunaangazia sababu kwanini unapaswa kuanzia mila hii iwapo bado hujaanza.
Manufaa ya kunywa maziwa kabla ya kulala

Kunywa kiwango kidogo cha maziwa ama bidhaa za maziwa kabla ya kuingia kitandani kumehusishwa na kulala vyema usiku.
- Kuboresha mizunguko yenye afya ya kulala
Maziwa huwa na melatonin na tryptophan, misombo inayosaidia kulala vyema. Tryptophan inasaidia katika utoaji wa serotonin inayosaidia kuboresha hisia, kupumzika na ina jukumu katika utoaji wa kisombo cha melatonin. Melatonin inafahamika kama kichocheo cha usingizi.
Baadhi ya wataalum wanashuku kuwa uwezo wa maziwa kusaidia kulala hakuhusiki na misombo ya virutubisho na badala yake, inahusika na athari za kifizikia za kuwa na mzunguko wa kimila. Kunywa glasi ya maziwa moto kabla ya kulala, huenda kukakukumbusha kuhusu kunywa maziwa kabla ya kulala ulipokuwa mchanga. Kuashiria akili yako kuwa ni wakati wa kulala.
Maziwa ama vinywaji vingine moto vinaponywiwa wakati wa fikira nyingi husaidia kupunguza mawazo, wasiwasi na kukufanya utulie.

Kunywa maziwa kabla ya kulala kutaathiri uzito wako?
Kula dakika chache kabla ya kulala kumehusishwa na ongezeko la uzito. Hata hivyo, kunywa glasi moja ya maziwa kabla ulale hakuwezi athiri pakubwa uzito wako, ikiwa haukunywi kila siku.
Kula kalori nyingi dakika chache kabla ya kulala kutaathiri mfumo wako wa kulala. Ikiwa kunywa glasi moja ya maziwa kabla ya kuingia kitandani kunakusaidia kulala vyema usiku kisha ushuhudie ongezeko la uzito. Huenda uzito huu unatokana na manufaa ya kulala vyema usiku.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Manufaa Ya Kula Kitunguu Saumu Kwa Afya Yako