Wataalum hushauri watu kuogelea kwa zaidi ya dakika 60 kila wiki. Je, kuna manufaa ya kuogelea? Kuogelea huwa na faida nyingi kwa mwili wote na mifumo tofauti ya mwili. Huwa mojawapo ya kupunguza uzito wa mwili kwa watu wanaolenga kuwa na uzani wa chini wa mwili.
Manufaa ya kuogelea

1.Kunakusaidia kudumisha uzani wenye afya
Kuogelea ni aina ya mazoezi yanayohusisha sehemu zote za mwili. Mabega, mikono, mgongo, miguu na tumbo. Ni aina ya cardio. Kwa watu wasioweza kufanya mazoezi ya aina nyingine, kuogelea kuna manufaa sawa.
2. Kuogelea kunakusaidia kuishi muda mrefu
Kulingana na utafiti, kufanya mazoezi kunaongeza muda unaoishi. Kuogelea ni aina ya mazoezi. Wataalum wa kuogelea wana hatari chini ya asilimia 28 za kifo cha mapema na chini ya asilimia 41 za kufariki kufuatia ugonjwa wa moyo ikilinganishwa na watu wasioogelea.
3. Kuboresha hisia zako
Baada ya kuogelea, hisia zako zitakuwa bora zaidi kufuatia kemikali za furaha zinazotolewa mwilini. Homoni hizi ni dopamine na serotonin zinamfanya mtu kuhisi vyema zaidi na kupunguza mawazo mengi.

4. Kuboresha afya ya moyo
Sawa na aina zingine za mazoezi, kuogelea kunaweza kusaidia kuimarisha uzima wa mfumo wa moyo. Kunasaidia moyo kuwa na nguvu na kuwezesha mapafu kutumia hewa vyema zaidi. Kuogelea kunawasaidia watu walio na matatizo ya shinikizo la damu na matatizo ya kimoyo.
5. Kuboresha nguvu za kiakili
Mazoezi husaidia kuboresha nguvu za kiakili. Kuogelea ni zoezi bora na huwasaidia watu kuongeza nguvu zao za kiakili. Kuogelea kwa dakika 20 hadi 30 kwa siku kunasaidia kuimarisha mfumo wako wa kiakili.
6. Kusaidia kupumzika na kulala vyema
Kufanya mazoezi kama vile kuogelea kunasaidia kulala vyema. Watu wenye umri mkubwa wanaotatizika kulala hupata ikiwa rahisi kulala baada ya kuogelea. Watu wanaotatizika na hali ya insomnia hulaa vyema baada ya mazoezi ya kuogelea kwa dakika 20 ama zaidi. Baada ya kuogelea utahisi vyema zaidi.
7. Kukabiliana na mawazo mengi
Kuogelea unapokuwa na mawazo mengi kumedhihirishwa kusaidia kuyapunguza. Baada ya kuogelea utahisi kuwa umepungukiwa na mawazo.
Kuogelea kuna manufaa mengi ya kiafya kwa mwili. Ni rahisi na huwa na bei isiyo ya juu. Ikiwa hauna maarifa ya kuogelea, ni vyema kuchukua darasa za kuogelea ama kuhakikisha kuwa kuna mtaalum kila mara unapoingia kwenye bwawa la maji.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Athari 5 Hasi za Sukari Kwenye Afya