Mipira ya kondomu ni baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinazotumika zaidi leo. Mbinu za uzazi wa mpango hulinda dhidi ya kupata ujauzito. Kutumia kondomu kuna linda dhidi ya kupata mimba. Mbali na kupata mimba, kutumia mpira wa kondomu kuna manufaa zaidi. Tazama manufaa ya kutumia kondomu.
Jinsi ya kutumia kondomu vizuri

Ili mpira wa kondomu utelekeze jukumu lake, unapaswa kuvaliwa ipasavyo. Kutotumia vizuri kuna muweka mwanamke katika hatari ya kupata mimba na maambukizi mengine. Hakikisha kuwa mpira haujapitisha siku za kutimiwa kwake na umevaliwa unavyohitajika.
- Toa mpira ule kwenye pakiti yake. Hakikisha kuwa hauharibiwi na kucha ama meno unapoutoa
- Valia kondomu kwa kibofu kilicho simama na kuhakikisha hakuna hewa kwenye mwisho wa kondomu
- Baada ya kutumia kondomu, itoe kwa kuvuta kutoka mwisho kwa umakini
- Itupe ifaavyo kwenye jalada
Manufaa ya mipira ya kondomu
- Ni rahisi kupata na kununua kondomu
- Ni rahisi kutumia ikilinganishwa na mbinu zingine
- Haina vichocheo vinavyoathiri mwili
- Haiathiri uzalishaji wa mwanamke ama mwanamme
- Inalinda dhidi ya maambukizi ya kingono kama vile kisonono na pia ukimwi
- Ina asilimia kubwa ya kulinda dhidi ya mimba na magonjwa inapotumika vizuri

Athari hasi za kutumia kondomu
- Msuguano zaidi ama friction wakati wa ngono unaweza kusababisha kuraruka kwa mpira wa kondomu na kusababisha mimba isiyotarajiwa
- Watu wanaotatizika kutokana na mzio wa latex huenda wakashindwa kutumia kondomu za kawaida
- Baada ya kumaliza tendo la ndoa toa kibofu kwenye uke wa mwanamke na utoe mpira huo kabla ya uume kurejelea hali ya kawaida na kumwaga shahawa ndani ya uke.
Wakati ufanisi wa kondomu huathiriwa
- Mpira wa kondomu unaporaruka
- Kondomu inapoharibiwa na mdomo ama kucha inapotolewa kwenye pakiti
- Kibofu kinapogusa uke kabla ya kuvalia kondomu
- Ikiwa mwanamme anatumia dawa kutibu hali kama thrush, huenda latex ya kondomu ikaathiriwa na kuathiri utendaji kazi wake
- Kondomu inapotoka katika kitendo cha ngono
Mahali kwa kununua kondomu
- Kliniki za uzazi wa mpango
- Kliniki za afya ya kingono
- Duka za dawa
- Duka kubwa ama supermarkets
- Stesheni za kuuza mafuta
Kutumia kondomu huwa na manufaa mengi, mbali na kulinda dhidi ya kupata mimba, mwanamke na mwanamme wanalindwa dhidi ya kupata maambukizi ya kingono kama kisonono na chlamydia.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Haya Yanafanyika Baada Ya Kufanya Ngono Kila Siku Kwa Mwaka Mzima