Mwanamke mjamzito anapaswa kuwa makini na chakula anachotia mdomoni. Ikiwa hana uhakika iwapo kitu fulani ni salama kuliwa, wakati ana mimba sio wakati bora wa kufanya majaribio haya. Matunda ni muhimu kwa afya ya mama mwenye mimba. Vitamini na madini katika matunda ni muhimu kwa afya yake. Tazama manufaa ya machungwa katika mimba.
Umuhimu Wa Kula Matunda Katika Mimba

- Yanasaidia kuboresha mfumo wa kinga
Machungwa yana kiwango cha juu cha vitamini C inayo saidia kuboresha mfumo wa kinga katika mama na mtoto anayekua kwenye uterasi. Machungwa yamedhihirishwa kuwa na madini ya iron na zinc ambayo yanachangia katika mfumo wa kinga kuwa na nguvu zaidi. Mwanamke mjamzito anashauriwa kula chungwa kila siku ili kupunguza athari ya kupata mzio anapokuwa na mimba.
2. Kupunguza ukosefu wa maji tosha mwilini
Mwanamke mjamzito hukumbana na tatizo la kukosa maji tosha mwilini, kwa kimombo constipation. Tatizo linalo sababishwa na baadhi ya vitamini anazo chukua katika mimba. Machungwa yana fibre na yanamsaidia mwanamke kutatua matatizo ya tumbo na pia kufura tumbo.

3. Kudhibiti viwango vya shinikizo ya damu
Machungwa yana viwango vya juu vya potasiamu inayo saidia kudhibiti shinikizo la damu mwilini mwanamke anapokuwa na mimba.
4. Kukuza ubongo wa mtoto
Folic acid na vitamini B6 iliyo kwenye machungwa inasaidia katika ukuaji wa ubongo wa mtoto. Folic acid inasaidia kuepusha kasoro za ubongo na uti wa mgongo katika watoto wachanga. Pia inasaidia katika kutengeneza seli za damu na tishu mpya.
5. Kuboresha ngozi ya mama
Matunda ya machungwa yana idadi ya juu ya maji inayosaidia mwili kuwa na maji tosha. Pia yana antioxidants zinazo ituliza ngozi na kuifanya ing'ae na kuepusha upele usoni.
Mwanamke anapaswa kula angalau machungwa matatu kwa siku. Iwapo atakula machungwa pamoja na vyakula vingine, ni vizuri kuwa makini na kiwango cha vitamini C katika vyakula hivyo. Kula idadi zaidi huwa na athari hasi kwa afya yake na ya mtoto. Machungwa yanaweza kuliwa wakati wowote, kutoka asubuhi hadi jioni.
Kwa wanao tatizika kula machungwa kavu, wanaweza kunywa sharubati freshi ya machungwa ili kunufaika kutokana na manufaa ya machungwa katika mimba. Epuka kuongeza sukari nyingi kwenye sharubati ya machungwa ili kusawazisha viwango vya sukari mwilini.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Je, Mwanamke Anaweza Kupata Ujauzito Bila Kujiingiza Katika Tendo La Ndoa?