Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Manufaa Ya Tendo La Ndoa Kwa Mama Mjamzito!

2 min read
Manufaa Ya Tendo La Ndoa Kwa Mama Mjamzito!Manufaa Ya Tendo La Ndoa Kwa Mama Mjamzito!

Wanawake wengi hufilisika kimawazo wanapokuwa na mimba. Kufanya mapenzi kumedhibitishwa kusaidia kutuliza akili na kupunguza mawazo mengi.

Kufanya mapenzi ukiwa mjamzito ni salama, kama ujauzito wako hauna matatizo yoyote na kama hujakatazwa na daktari ama mkunga wako. Kufanya mapenzi katika kipindi hiki pia kuna manufaa mengi kwa mama. Tazama orodha yetu ya manufaa ya ngono kwa mama mjamzito.

Manufaa Ya Ngono Kwa Mama Mjamzito

manufaa ya ngono kwa mjamzito

  1. Kupona ni rahisi zaidi

Kufanya mapenzi unapokuwa na mimba kunafanya uchungu wa uzazi na kupona baada ya kujifungua kuwe rahisi zaidi. Kufika kilele mara kwa mara kuna boresha kubanwa kwa pelviki na kusaidia kuipa misuli yako nguvu tosha utakayo ihitaji katika mchakato wa uchungu wa uzazi.

Baada ya kujifungua, misuli hii bado ina nguvu na kumsaidia mama kupona kwa kasi.

2. Kupunguza shinikizo la damu

Shinikizo la damu lina husiana na mimba hasa mama anapo karibia kujifungua. Kufanya ngono mara kwa mara katika mimba kutapunguza hatari ya mama kutatizi na preeclampsia. Hii ni aina ya tatizo la mimba linalo ashiriwa na shinikizo la juu la damu na ishara za kuharibika kwa viungo vingine. Kwa wanawake wanao tatizika na hali hii, ishara zake huanza kuonekana wanapo timiza wiki ya 20 ama ya 21 ya safari yao ya ujauzito.

3. Kumtayarisha mama kwa uchungu wa uzazi

Mama anaweza kufika kilele kwa kasi anapo fanya mapenzi akiwa na mimba. Anapo fika kilele, uterasi inabanwa na kufanya iwe rahisi kwake kusukuma anapo kuwa katika mchakato wa uchungu wa uzazi. Ikiwa mimba yako haina tatizo, usione haya kufanya mapenzi hadi pale utakapo jifungua.

4. Kumsaidia mama kufika kilele

manufaa ya ngono kwa mjamzito

Mama anapokuwa mjamzito, viungo vyake vya mwili huwa nyeti sana. Hasa viungo vinapo tumika kumsisimua katika tendo la ndoa kama vile chuchu. Kwa hivyo, inakuwa rahisi zaidi kwa mama kufika kilele wakati wa kufanya mapenzi.

5. Ni zoezi

Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mwenye mimba. Mbali na kusaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini, viungo vya mwili wake vinafanya mazoezi na pia kupunguza uchungu katika sehemu tofauti za mwili wake.

6. Kupunguza mawazo mengi

Wanawake wengi hufilisika kimawazo wanapokuwa na mimba. Kufanya mapenzi kumedhibitishwa kusaidia kutuliza akili na kupunguza mawazo mengi. Kwa hivyo unapokuwa na mawazo mengi ukiwa mjamzito, hii hapa ndiyo dawa bora.

Usiwe na shaka unapofanya mapenzi katika mimba, na kuogopa kuwa huenda mtoto aka athiriwa.

Soma pia: Mama Anapaswa Kungoja Muda Upi Kufanya Ngono Baada Ya Kujifungua?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Manufaa Ya Tendo La Ndoa Kwa Mama Mjamzito!
Share:
  • Ni Wakati Upi Ambapo Mama Hapaswi Kufanya Ngono Akiwa Na Mimba?

    Ni Wakati Upi Ambapo Mama Hapaswi Kufanya Ngono Akiwa Na Mimba?

  • Ni Salama Kwa Mama Mjamzito Kujihusisha Katika Tendo La Ndoa?

    Ni Salama Kwa Mama Mjamzito Kujihusisha Katika Tendo La Ndoa?

  • Tendo La Ndoa Ni Bora Kwa Afya Na Uhusiano Wako: Kwa Njia Hizi

    Tendo La Ndoa Ni Bora Kwa Afya Na Uhusiano Wako: Kwa Njia Hizi

  • Mambo Muhimu Ya Kufanya Baada Ya Tendo La Ndoa!

    Mambo Muhimu Ya Kufanya Baada Ya Tendo La Ndoa!

  • Ni Wakati Upi Ambapo Mama Hapaswi Kufanya Ngono Akiwa Na Mimba?

    Ni Wakati Upi Ambapo Mama Hapaswi Kufanya Ngono Akiwa Na Mimba?

  • Ni Salama Kwa Mama Mjamzito Kujihusisha Katika Tendo La Ndoa?

    Ni Salama Kwa Mama Mjamzito Kujihusisha Katika Tendo La Ndoa?

  • Tendo La Ndoa Ni Bora Kwa Afya Na Uhusiano Wako: Kwa Njia Hizi

    Tendo La Ndoa Ni Bora Kwa Afya Na Uhusiano Wako: Kwa Njia Hizi

  • Mambo Muhimu Ya Kufanya Baada Ya Tendo La Ndoa!

    Mambo Muhimu Ya Kufanya Baada Ya Tendo La Ndoa!

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it