Faida Za Kiafya Za Kula Njugu Usizo Zifahamu

Faida Za Kiafya Za Kula Njugu Usizo Zifahamu

Japo kuwa watu wengi hawa fahamu, njugu ni mojawapo ya vyanzo bora vya protini na zina manufaa mengi ya kiafya. Pia, zina wingi wa ufuta mzuri. Njugu, ama siagi ya njugu zina magnesium, copper, ariginine, vitamin e na foliate. Na zina fahamika kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya cardiovascular.

Kulingana na masomo ya hivi majuzi, ngozi ya njugu ina kiwango cha juu cha antioxidants asili na fiber. Tazama manufaa zaidi ya kula njugu.

Tazama manufaa haya ya kula njugu:

Faida Za Kiafya Za Kula Njugu Usizo Zifahamu

  1. Wingi wa antioxidant

Ngozi ya njugu ina bidhaa za phenolic na kumaanisha kuwa zina antioxidants nyingi. Ambazo zina linda mwili kutokana na hatari za magonjwa na saratani. Kulingana na utafiti, kusiaga njugu zenye ngozi kuliongeza viwango vya antioxidants kwenye siagi hiyo kwa asilimia 5.

2. Ufuta wenye afya ya moyo

Njugu zina aina ya ufuta unao julikana kama monounsaturated na polyunsaturated unao saidia moyo kuwa na afya. Na ni muhimu sana kwa afya ya moyo kwa sababu ya ufuta huo unaosaidia kupunguza viwango vya kolesteroli kwenye damu na aina zingine za magonjwa ya moyo.

3. Chanzo kizuri cha protini

Inapofika kwa afya ya seli zetu, protini ni muhimu. Na hii ni kwa sababu seli zilizo kwenye miili yetu mara kwa mara zinabadilishwa na kutengenezwa kuhakikisha kuwa seli mpya zina afya na zilizo haribika zina tengenezwa pia. Mahitaji ya protini hayawezi sisitizwa vya kutosha. Kufuatia wingi wa protini kwenye njugu, wataalum wa afya wana sisitiza umuhimu wa kuziongeza kwenye lishe ya watoto, watu wazima, wanao kosa madini fulani, na wasio kula nyama.

4. Chanzo kikuu cha madini

njugu

Kama tulivyo angazia mwanzoni, njugu ni chanzo chanzo kikuu cha madini. Na baadhi ya madini haya ni kama vile magnesium, zinc, kalisi, potassium, sodium, na phosphorous. Madini haya ni muhimu kwa utendaji kazi wa miili yetu. Na pia yanasaidia kuhakikisha afya ya mitima yetu iko shwari.

5. Wingi wa madini

Vitamini ni muhimu sana katika ukuaji na maendeleo ya kijumla. Vitamini zina hakikisha ukuaji wa kijumla wa seli na tishu mwilini na pia kupigana dhidi ya maambukizi na kuhakikisha kuwa viungo vya mwili zina fanya kazi inavyo faa.

Soma PiaOrodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

Written by

Risper Nyakio