Tangawizi ni kiungo maarufu jikoni. Ila kuna baadhi ya watu wasio fahamu manufaa yake. Kina ongeza ladha ya kuvutia kwenye chakula na pia huwekwa ndani ya chai. Kuipa ladha zaidi. Hata hivyo, huenda kuna watu wanacho kitumia kiungo hiki bila kufahamu manufaa ya tangawizi kwa afya yake. Leo tunaangazia faida zake na pia mabadiliko yanayo tendeka mwilini mtu anapokula tangawizi kila siku. Soma zaidi!
Manufaa Ya Tangawizi Kwenye Afya
- Kukomesha ukuaji wa seli za saratani

Kiungo cha tangawizi kimedhihirishwa kuwa na uwezo wa kupunguza na kukomesha ukuaji wa seli za baadhi ya aina za saratani kama vile, ya ngozi, matiti, maini na gastric. Utafiti zaidi unazidi kufanyika kuegemeza hili.
- Kutuliza misuli inayo uma
Tangawizi hutumika sana na wana michezo. Baada ya kujihusisha na michezo ya aina yoyote iliyo na mazoezi makali, misuli ya mwili huumia. Tangawizi inasaidia kutuliza misuli.
Kiungo hiki kina uwezo wa kupigana dhidi ya viini vinavyo sababisha magonjwa, bakteria na virusi kama RSV.
- Kupunguza kolesteroli mwilini
Kiwango kidogo cha tangawizi kinasaidia kupigana dhidi ya kolesteroli mbaya mwilini.
Kiungo hiki kina epusha vimelea kukua kwenye mdomo. Vimelea hivi vina husishwa na maambukizi ya ufizi.
- Kupunguza uchungu katika hedhi

Binti anapo shuhudia siku zake za hedhi, na kuhisi uchungu mwingi, anashauriwa kunywa maji yaliyo na tangawizi. Kijiko kimoja cha powda ya tangawizi kwenye kikombe kimoja cha maji moto kitasaidia kupunguza uchungu huo.
- Kulinda dhidi ya magonjwa
Tangawizi ina linda mwili kutokana na magonjwa kama vile shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa moyo, maradhi ya mafua na kuepusha kuzeeka kwa kasi.
Mbali na faida tulizo angazia za kiungo hiki, tangawizi ni muhimu kwa mama mwenye mimba. Anapo iongeza kwenye maji yake ya kunywa, ina punguza kichefu chefu na hisia ya kutapika kila mara.
Kuvimba miguu ni maarufu kwa wanawake wenye mimba, tangawizi inasaidia kupunguza kufura huku.
Soma Pia: Kutengeneza Uhusiano Na Mtoto Ukiwa Na Mimba Na Manufaa Ya Kiafya