Mwathiriwa Wa Ajali Ya Ndege Ya Sosoliso, Kechi Okwuchi Akumbuka Walio Aga

Mwathiriwa Wa Ajali Ya Ndege Ya Sosoliso, Kechi Okwuchi Akumbuka Walio Aga

Tarehe 10 mwezi wa Disemba, Kechi Okwuchi, mojawapo wa manusura wa ajali ya ndege ya Sosoliso, alikumbuka siku ambayo karibu aage dunia miaka 15 iliyo pita.

Miaka 15: Manusura wa Ajali ya Ndege ya Sosoliso 

Kechi okwuchi

Kechi Okwuchi, ambaye ana miaka 30, alienda kwenye kurasa yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter kukumbuka siku ambayo angekufa miaka 15 iliyo pita. Alikuwa mojawapo ya wanafunzi 61 wa sekondari ya Loyola Jesuit College wakielekea nyumbani kusherehekea likizo ya Krismasi. Kulikuwa na watu 110 kwenye ndege hiyo ya Sosoliso Disemba 10, 2005. Kwenye ujumbe wa twitter wa Kechi, alikumbuka walio yapoteza maisha yao katika ajali hiyo. Huku akimshukuru Maulana kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi kwa walio yapoteza maisha yao siku hiyo.

twitter.com/Kechi/status/1204332119138418688?s=20

 

Aliandika: "Siku hii miaka 15 iliyo pita, maisha yangu karibu yafike kikomo katika umri wa miaka 16. Leo nina miaka 30 na nina mshukuru Mualana kwa kunikubalisha kuishi kwa watu walio poteza maisha yao mnamo tarehe 10 mwezi wa Disemba 2005. Nina shukrani kwenu nyote kwa msaada na uegemezo mlo nipa huku nikiendelea kuishi ndoto zangu. RIP malaika #hamtasahaulika."

Mwathiriwa Wa Ajali Ya Ndege Ya Sosoliso, Kechi Okwuchi Akumbuka Walio Aga

Walakini, kuna manusura mwingine anaye julikana kama Bunmi Amusan katika wakati wa ajali hiyo ya ndege. Bunmi alikuwa msaidizi mdogo wa mhubiri wa kike Bimbo Odukoya, aliyekufa kufuatia majeraha siku chache baada ya ajali hiyo. Bunmi alioleka miezi miwili baadaye kwa Jide Adams, aliyekuwa mfanyakazi wa Cornerstone Insurance na muabudu wa kanisa la Fountain of Life Church. Katika wakati huo, habari kuhusu mipango ya harusi yao ilibaki siri. Na wana habari wachache walio taka kupata habari kuhusu harusi hiyo walitoka mikono mitupu. Kutoka ajali hiyo, amebaki na maisha fiche sana na sio mengi yanayo julikana kumhusu.

Ni furaha yetu kuwa manusara wa ajali hiyo ya ndege wanaendelea vizuri na kuendelea kutimiza ndoto zao maishani.

manusura wa ajali ya ndege ya sosoliso ,kechi okwuchi

 

Soma piaPlane Crash Survivor, Kechi Okwuchi Celebrates Her 30th Birthday In Style

 

Written by

Risper Nyakio