Mapacha Abby Brittany Hensel Walio Shikana Kwenye Kifua

Mapacha Abby Brittany Hensel Walio Shikana Kwenye Kifua

Abigail Loraine Hensel na Brittany Lee Hensel ni mapacha walio zaliwa mnamo mwaka wa 1990 mwezi wa tatu tarehe 7 Minnesota huko Umerikani. Mapacha hawa walizaliwa huku wameshikana na wanajulikana kama Abby Brittany Hensel. Wana mwili mmoja usio na alama za tofauti ila kila mmoja ana viungo tofauti za mwili ambazo hawa tumii pamoja.

Abby Brittany Hensel walipata umaarufu mwaka wa 1996 walipo onekana kwenye kipindi maarufu cha Oprah Winfrey kinacho julikana kama “The Oprah Winfrey Show” mwezi wa Aprili tarehe 8 na 29 mwezi huo huo. Kila mtu alitaka kujua zaidi kuhusu mapacha hawa na jinsi wanavyo ishi na kufanya kazi zao za kila siku. Na hivi wakajulikana na watu na kufungua milango yao ya kutokea kwenye vipindi vingine.

Kila mmoja wa mapacha hawa ana mkono mmoja na mguu. Kama watoto wadogo, walijifunza kukaa, kutambaa na kupiga makofi kwa pamoja. Ila, mambo kama vile kukula na kuandika, wanafanya kitofauti. Shughuli zingine kama kukimbia, kuogelea na kuchana nywele na pia kuendesha gari, wawili hawa lazima wafanye kwa pamoja.

Mapacha Abby Brittany Hensel Walio Shikana Kwenye Kifua

Je, Unaifahamu Fizikia ya Abby Brittany Hensel ?

Mapacha hawa wana mwili mmoja na shingo na vichwa tofauti, mikono na miguu miwili. Kwa sababu wameshikana, kifua chao ni kikubwa kupiku ilivyo kawaida. Walipozaliwa, kulikuwa na mkono mdogo kati ya shingo zao ila upasuaji ulifanyika kutoa mkono huo na kubakisha mikono miwili. Wazazi wao Mike na Patty Hensel walikataa mapacha hawa kufanyiwa upasuaji kuwatenganisha. Kwani kulikuwa na hatari nyingi na huenda wawili hawa wange kosa kuishi baada ya upasuaji ule kufanyika.

Abby ako upande wa kulia ilhali Brittany ako upande wa kushoto. Walipokuwa miaka 12, walifanyiwa upasuaji  ili kupanua  kifua chao kuepuka matatizo ya usoni ya kupumua. Brittany ni mfupi kidogo kuliko Abby na uti wa mgongo wa Abby ulisimamishwa kukua baada ya Brittany kukosa kukua ili kuhakikisha kuwa mili yao inakua pamoja na hakuna aliye na mwili uliokomaa zaidi ya mwingine kwani ingekua vigumu kutangamanisha shughuli zao kama mapacha.

Kila mmoja wa mapacha hawa anathibiti upande wake wa mwili. Ila kwa mambo yanayo hitaji nishati zao wawili, lazima watangamane. Kama vile kutembea, kuogelea, kukimbia na kuendesha baiskeli ama gari.

Mapacha Abby Brittany Hensel Walio Shikana Kwenye Kifua

Viungo vya mwili kwa mapacha hawa

Mapacha hawa wana viungo tofauti vya mwili wa juu na viungo vya chini wana tumia kwa pamoja. Tuna angazia kwa kina sehemu tofauti za mapacha hawa.

 • Vichwa viwili
 • Uti wa mgongo kwa kila mmoja wao.
 • Mkono mmoja kwa kila mmoja wao
 • Kifua kilicho panuka
 • Matiti 2 kila mmoja
 • Mioyo miwili
 • Mapafu 4
 • Tumbo mbili
 • Vibofu vya mkojo viwili
 • Ini moja
 • Figo tatu (mbili upande wa kushoto na moja upande wa kulia)
 • Utumbo mkubwa 1
 • Utumbo mdogo 1
 • Miguu miwili

abby brittany hensel

Utu Uzima wao

Mapacha hawa Abby Brittany Hensel wali hitimu kutoka shule ya upili mwaka wa 2008 na baadaye kujiunga na Chuo Kikuu cha Bethel kilichoko Minnesota. Walisomea B.A Arts na kuhitimu mwaka wa 2012. Walitaka kuwa walimu walipokua ili waweze kuwafunza wengine na kuwapa wengine mwelekeo chanya kwenye maisha yao. Pia wangetaka kupata wachumba kila mmoja na baadaye kupata watoto. Baadhi ya nguo zao, lazima zitengenezwe ili ziweze kuwatoshea vyema kwenye shingo. Brittany na Abby Hensel huvalia viatu tofauti. Huenda ukapata kuna siku kila mmoja amevalia kiatu cha rangi tofauti.

 

Written by

Risper Nyakio