Mama Wa Miaka 68 Ajifungua Mapacha Huko LUTH Nigeria

Mama Wa Miaka 68 Ajifungua Mapacha Huko LUTH Nigeria

Mwanamke wa miaka 68 amejifungua mapacha kupitia IVF katika Lagos University Teaching Hospital, Idi-Araba. Mwenyekiti wa baraza la Ushauri wa Matibabu la Luth, profesa Wasiu Adeyemo; alisema kuwa mwanamke huyo alikuwa mjamzito kwa mara yake ya kwanza baada ya In Vitro Fertilisation.

Alisema kuwa "LUTH imefanyikisha kujifungua kwa mwanamke wa miaka 68 iliyo kuwa mara yake ya kwanza kujifungua, mapacha (wa kike na kiume) kufuatia msaada wa kutunga mimba wa IVF.

"Alijifungua kupitia njia ya upasuaji wa C-section katika wiki 37 za mimba tarehe 14, mwezi wa Aprili 2020".

twins by ivf

"IVF na uhamisho wa kiinitete ulifanyika katika kituo cha nje. Na baadaye akatumwa LUTH katika hatua za mapema za gesti na kuhudumiwa hadi akamaliza. Hii ni mara ya kwanza LUTH huko Nigeria na Africa! Mama na watoto wote wako salama."

IVF ni njia ya kusaidiwa kutunga mimba kutumia teknolojia inayo husisha kutoa mayai kutoka kwa ovari za mwanamke na kuzi pevua na manii.

Kulingana na Profesa Adeyemo, hii ni mara ya kwanza kisa kama hicho kitashuhudiwa Afrika.

Walakini, kuna rekodi ya mama wa miaka 74 kujifungua huko kusini mwa India.

Mangayamma Yaramati alipata mimba kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua kwa kupitia invitro fertilisation. Pia alijifungua mapacha, wote wasichana kupitia upasuaji wa C-section.

Katika mwaka wa 2015, mwanamke wa miaka 56 huko Ujerumani, Annegret Raunigk, aliyekuwa tayari na watoto 13 alijifungua quadruplets baada ya kutunga mimba kupitia na kujifungua watoto wanne baada ya kutunga mimba kupitia artificial insemination huko nchi ya Ukraine.

Kuna maana gani kupata mapacha kupitia IVF?

mom of multiples

IVF (inayo simamia In vitro fertilization) ni teknolojia ya kupata watoto kupitia usaidizi wa kiteknolojia inayo saidia kutunga mimba, kukua kwa kiinitete, na kujishikilia kwenye kuta za uterasi. Kwa urahisi, ni kusaidia wanandoa kupata mimba.

Hivi ndivyo inavyofanya kazi: madaktari hutoa ovari za mwanamke na manii ya mwanamme na kuzileta pamoja kwenye maabara ya kimatibabu. Ili kukubalisha manii kupevua mayai. Kutunga kunapo tendeka, kiinitete kinaanza kukua na wataalum kuiweka kwenye uterasi.

Hapa chini kuna baadhi ya sababu za kawaida sana kwanini baadhi ya watu hutumia IVF:

  • Kwa kesi ambazo ovari hufeli, kuwa na fibroids kwenye uterasi na matatizo ya kutunga na kadhalika.
  • Endometriosis
  • Kutaka watoto zaidi ya mmoja
  • Kwa kesi ambapo kuna fallopian tubes zilizo fungika.
  • Iwapo moja wapo kati ya wanandoa ana matatizo ya kijeni ambayo hawati kupitisha kwa watoto wao.
  • Iwapo tube za fallopian zilitolewa kupitia upasuaji.
  • Mwanamme anakumbana na tatizo la kuwa infertile kama vile kiwango cha chini cha manii na kadhalika.
  • Kesi zingine za kuto dhibitika kwa infertility.
  • Umri na kutimiza miaka ya kutopata mtoto.

IVF kama njia ya kujifungua saidizi kupitia teknolojia imekuja njia ndefu. Kumekuwa na kuimarika na mafanikio makubwa na ya kiwango cha juu ikilinganishwa na karne iliyo pita.

Hisia za watu kuhusu utaratibu huu pia zimebadilika. Watu wengi kwa sasa wanajua zaidi kulingo kuwa tenga wanandoa wanao tumia teknolojia hii. Karibu kila mtu anajua mtu aliyepitia utaratibu huu na watu wamejua jinsi ya kuwaegemeza na kuwapa moyo wanandoa wanao chagua njia hii ya kupata watoto. Na hii ni hatua kubwa hasa kwa jamii nyingi zilizo kuwa na mtazamo hasi kuhusu utaratibu huu.

Ukiamua kufuata utaratibu wa IVF, haimaanishi wewe ni mja mdogo. Iwapo kuna lolote, kuna maana wewe ni jasiri, una akili wazi na ume elimika.

Guardian NG

Soma pia: IVF Procedure: Nigerian Mom Shares Her Egg Retrieval Experience

Written by

Risper Nyakio