Mama anapojifungua, anaanza maisha mapya na kukikaribisha kiumbe kingine maishani na nyumbani mwake. Maisha haya mapya huwa na mabadiliko mengi. Hasa kama ni mama wa mara ya kwanza, angali anajifunza jinsi ya kumtunza mtoto na kurekebisha ratiba yake iandamane na ratiba ya kulala kwa mtoto. Katika kipindi hiki, mama ana mawazo mengi, kumtunza mtoto, kumlisha, kumnyonyesha, kumbadili nepi, na huenda akawa hana hamu ya mapenzi baada ya kujifungua. Na hata ikiwa anayo, iko chini sana kwani nishati nyingi inatumika kumtunza mtoto. Mbali na hayo, angali anapona kutokana na kujifungua na ni vyema kuchukua muda kupona kabla ya kurejelea tendo la ndoa.
Kuzungumza na mchumba wako kuhusu ngono baada ya kujifungua

Kuwa na mazungumzo wazi na mchumba wako ni muhimu katika kipindi hiki. Huenda wakahisi kana kwamba mtoto amechukua nafasi yao na hawapati muda na bibi zao tena. Mama anaweza fanya mambo haya:
Kuzungumza kwa uwazi. Mweleze mchumba wako unavyo hisi kuhusu ngono baada ya kujifungua. Unacho ogopa, unacho kifurahia na umweleze unapohisi kuwa utakuwa tayari kufanya mapenzi tena.
Mweleze unachotaka. Je, ungependa kufanya mapenzi wakati huu, ama vitendo vingine vya kimapenzi. Kumbuka kuwa mpenzi wako pia ana mahitaji yake, mpe sikio anapokueleza anachotaka pia.
Upe mwili wako muda upone. Miili ya wanawake ni tofauti na huchukua muda tofauti kupona baada ya kujifungua. Usikilize mwili wako. Ukihisi kuwa unahitaji muda zaidi kabla ya kurejelea kufanya mapenzi, ni sawa.
Njia zingine za kuwa karibu na mchumba wako bila ngono

Kuna njia nyingi ambazo wanandoa wanaweza kuwa na utangamano bila ya kufanya mapenzi. Kama vile:
Kuwa na wakati pamoja. Ni vyema kwa wanandoa kuhakikisha kuwa wanazidi kupata chanya cha kuwa peke yao, mbali na kumtunza mtoto. Hata dakika chache kwa siku, kuzungumza kuhusu jinsi siku zao zimekuwa.
Busu. Wakati ambapo kufanya ngono hakuwezekani hasa siku za kwanza baada ya kujifungua, wazazi wanaweza jaribu kuonyeshana mapenzi kwa njia zingine kama kubusiana.
Kumtunza mwenzi wako. Mchumba wa kiume anaweza jaribu kumtunza bibi yake kwa kumfanyia vitu vidogo vinavyo mjaza na furaha kama vile kumkanda miguu, kumsaidia kumbadili mtoto nepi ili mama apate wakati wa kupumzika. Ni vitendo hivi vidogo vinavyo mhakikishia kuwa angali anapendwa na kudhaminiwa. Na hata kama mngali hamjarejelea mapenzi baada ya kujifungua, atahisi mapenzi yako kwake.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Kwa Nini Watu Wasio Na Usawa Hawawezi Kuwa Na Uhusiano Wa Kimapenzi?