Mambo Ya Kufanya Mapenzi Yanapo Isha Katika Ndoa

Mambo Ya Kufanya Mapenzi Yanapo Isha Katika Ndoa

Jinsi ya kufufua ndoa mapenzi yanapo isha.

Mapenzi yanapo isha katika ndoa, matokeo huenda yaka athiri uhusiano sana iwapo wanandoa hawataki kutia juhudi kufufua uhusiano wao. Kwa kukosa uhusiano wa ndani, hatumaanishi ndoa tu. Uhusiano wa kihisia ni muhimu muhimu kwa ndoa yoyote.

Uhusiano hauji na kuisha tu katika ndoa. Iwapo wanandoa wenye tatizo hili wanachukua wakati kufikiria kwa makini chanzo chake, watagundua kuwa kufifia kwa uhusiano hakukutendeka tu. Ni mchakato wa polepole unao ingia na kuongezeka kwa kipindi cha muda.

Kwa hivyo, uhusiano huishi hivyo tu katika ndoa?

Mapenzi yanapo isha katika ndoa: Sababu huenda zikawa!

1. Kukosa uhusiano wa kifizikia na hisia

Uhusiano wa kimapenzi/kingono hufifia punde tu wachumba wanapo acha kuhusiana kifizikia. Hili hutendeka wanapo koma kuwa na wakati pamoja. Ngono huenda ikaonekana kama kazi yoyote ile, na katika visa vilivyo zidi, ngono huenda ikaisha pamoja.

when intimacy dies in marriage
2. Mawazo mengi

Mawazo mengi huwa miongoni mwa sababu za kukosa uhusiano katika ndoa. Hamu ya kingono huenda ikaisha pale ambapo mke ama mume ana kwazwa kifikira. Ukigundua kuwa uhusiano wenu katika ndoa umepunguka, unaweza fanya utafiti kujua chanzo cha vikwazo hivi -  huenda ikawa ofisini ama hata nyumbani mwenu.

3. Kuto jithamini kwa sana ama kuto jua thamana yako

Madhara ya kukosa uhusiano katika ndoa huenda ikawa ni kufuatia kuto jithamini. Iwapo mwanamme ama mwanamke anahisi kuwa na shaka kuhusu mwili wake ama kuwa hapendezi, huenda wakakua kuchukia hali yao na kuanza matatizo. Shida hii hupiku wasipo kumbushwa kuwa wanapendeza na wachumba wao. Yoyote anaye hisi kuwa hapendezi huenda akakosa hamu ya kuvua nguo na kufanya mapenzi na mchumba wake.

4. Kuhisi kukataliwa na kuto pendwa

Hakuna mtu anayepaswa kuhisi kuwa hapendwi. Baadhi ya wakati, kukataliwa huenda kukawa na athari hasi. Huenda anaye fanya hivi akakosa kugundua anapo fanya hivi na wakati mwingine akafanya hivyo kimaksudi. Usikatae mchumba wako mara kwa mara kwani hujui kiasi ambacho itakavyo waathiri. Jaribu kuwahimiza wanapo jaribu vitu vipya kitandani ama wanapofanya juhudi za kufanya maisha yenu ya kindoa yawe na ladha zaidi.

when intimacy dies in marriage
5. Chuki ya muda mrefu

Sababu nyingine ya kukosa uhusiano wa karibu katika ndoa ni kuwa na chuki. Chuki isipo zungumziwa, huenda ikakua kuwa kitu kikubwa na kuto taka kuwa karibu na mchumba wako.

6. Kuzoea kitu moja kwa muda mrefu

Wanandoa walio funga ndoa kwa wakati mrefu wata kuambia kuwa iwapo haufanyi juhudi za kuongeza ladha katika maisha yako ya kindoa, ngono huenda ikawa ya kawaida na ya kuchosha. Mara tu uzoefu huu unapo anza, hamu ya ngono huenda ikafifia kwa sababu hautarajii kitu kipya chumbani chenu cha kulala. Hii ni mojawapo ya matokeo ya kukosa uhusiano katika ndoa yenu.

7. Uchungu na kuumizwa hapo awali

Cha kuhuzunisha ni kuwa, mawazo ya matukio ya hapo awali huenda yakaanza kurudi usipo yatarajia. Sio vigumu kwa mtu kujitenga na njia zote za mapenzi wakikumbuka kitu kilicho tendeka hapo awali. Mawazo ya matukio ya mahusiano ya hapo awali huenda yaka sababisha mchumba wako kujitenga mbali nawe kihisia na kimapenzi.

mapenzi yanapo isha katika ndoa
Mapenzi yanapo isha katika ndoa

Kama tulivyo taja hapo awali, kukosa ngono katika ndoa huenda kuka haribu ndoa iwapo hakuna jambo la dharura linalo fanywa. Uhusiano unapo endelea kufifia, yafuatayo huenda yakafanyika katika ndoa:

• Kutoka nje ya ndoa

Kutoka nje ya ndoa huwa na uwezekano wakati ambapo wanandoa hawapati ngono tosha kutoka kwa wachumba wao. Hii sio sababu ya kutoka nje, ila ni uwezekano mkubwa wa kutafuta ngono kwingine usipo ipata nyumbani.

Kupeana talaka

Asilimia ya kuwachana kwa wanandoa inaendelea kuongezeka kila siku. Hata kama hakuna aliye jaribu kufanya utafiti kudhibitisha ni wachumba wangapi walio tengana kufuatia kuwa na ndoa bila ngono, uwezekano uko juu sana.

Kuchukiana

Kuna vitu vichache vya kuhuzunisha kama wanandoa walio anza safari yao wakipendana sana na baadaye kukua kuchukiana. Mtu mmoja anapo anza kuhisi kuwa hapendwi na hatakikani kwa sababu ya kukosa mapenzi, huenda wakaanza kuchukia wenzi wao.

Mazungumzo yanaweza athirika

Madhara ya kuwa na uhusiano usio na mapenzi huwa kama vile mazungumzo masikini. Umbali wenyewe huenda ukafanya iwe vigumu kwa baadhi ya wanandoa kuongea kwa uwazi kuhusu hisia zao. Mazungumzo yanapo feli katika ndoa, ndoa ni kama imeisha.

• Kuto jithamini

Kuto jithamini huenda kukaua uhusiano wenu katika ndoa, na kuleta madhara mengi. Mtu anayetaka kufanya mapenzi ila anapatana na mwenzi asiye itikia mwito huo kila mara anapo anzisha, huenda akapata matatizo ya kuto jithamini. Katika kesi hii, ni asili kushangaa iwapo mwenzi wako haitikii mwito wako kwa sababu humpendezi kifizikia. Watu katika ndoa bila ngono huenda wakapoteza hamu ya kujithamini iwapo hawako makini kuangazia hisia zao kwa kina.

Mapenzi yanapo isha katika ndoa: Jinsi ya kusuluhisha tatizo hili

Kuna uwezekano wa kuregesha mapenzi katika uhusiano wenu. Ila ili jambo hili lifanyike lazima utie bidii na juhudi nyingi. Mchakato wa kuregesha mapenzi katika ndoa huenda ikawa ngumu hapo mwanzoni, ila lina wezekana!

Hapa kuna baadhi ya njia ambazo unaweza tumia kuregesha mapenzi yenu:

 

1. Tafuta ushauri

Ushauri unaweza kusaidia kujua zaidi kuhusu hisia na matatizo yaliyo fanya mapenzi katika ndoa yenu iishe. Ushauri wa ndoa unaweza fanya mapenzi yenu yarudi.

2. Thamini mwenzi wako

Maneno yako ya kuhamasisha zinaweza saidia sana katika kumfanya mwenzi wako ahisi kuwa ana pendwa na kuthaminiwa. Mwenzi anaye hisi kuwa ako salama katika uhusiano hatakuwa na uwoga kukueleza kinacho msumbua.

3. Jadili matitizo yoyote kabla yawe makubwa

Usikubali hasira ziongezeke kwa kiwango ambacho kita athiri harusi yenu. Ondoa hisia zozote zile za chuki kabla ya vitu kuwa mbaya.

Huffington Post

Soma pia: The 7 erogenous zones in women husbands should know about

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio