Mojawapo ya wakati wa kusisimua zaidi katika safari ya ujauzito kwa mama ni anapohisi mpigo wa mtoto. Huwa ishara ya mapema kuwa mama ana kiumbe kinachokua ndani yake. Mama anapohisi mpigo wa kwanza, hujazwa na furaha na hisia tele, huenda pia akawa na shaka. Yote haya ni sawa. Mapigo ya mtoto ni njia ya kukuhakikishia kuwa anakua vyema. Mama mjamzito huenda akawa na maswali tele, kama vile, je, mapigo ya moyo ya mtoto tumboni huanza muda gani? Katika makala haya, tuna angazia muda ambapo mtoto huanza kuwa na mapigo.
Mapigo ya mtoto tumboni huanza muda gani

Mtoto huanza kurusha mateke tumboni unapokuwa kati ya wiki 18 hadi 20 za ujauzito. Ikiwa hii ni mara ya kwanza ya mama kupata mimba, huenda akakosa kufahamu mapigo haya kwani huwa mepesi sana. Hii ni njia ya mtoto kuanza mazungumzo na mamake. Mama asiyefahamu hili, huenda akadhani ana tatizo la gesi.
Sababu zinazomfanya mtoto kuwacha kucheza tumboni
- Mama kuchoka sana baada ya kufanya kazi nzito. Mtoto atahitaji kutulia apumzike pia
- Kukosa nguvu na nishati tosha kufuatia lishe hafifu ya mama
- Mama kutatizika na maradhi ya kiafya. Mtoto hukosa nishati tosha ya kucheza
- Baada ya mama kutembea kwa muda mrefu, mtoto atakosa kucheza kwani yeye pia amechoka
- Mtoto kuwa na uzani wa chini na umbo ndogo
- Mtoto kufariki
Jinsi ya kumfanya mtoto acheze

Mama anaweza kuchochea kucheza kwa mtoto kwa kufanya haya:
- Kunywa maji baridi
- Kula chakula kilicho na sukari nyingi
- Kula chakula chenye pilipili
- Kuzungumza na mtoto
- Kulala kwa upande wa kushoto, utaweza kuhisi mwendo wa mtoto
Kadri ujauzito unavyozidi kukua, ndivyo unavyohitajika kuwa makini na mwendo wa tumboni wa mwanao. Kufahamu iwapo ako hai zaidi asubuhi, mchana ama jioni. Hakuna nambari hasa ya mateke ambayo mtoto anapaswa kurusha kwa siku. Lakini ukigundua kuwa idadi ya mara ambayo mtoto wako hupiga imepungua, wasiliana na daktari wako.
Unapokuwa na shaka kuhusu mapigo ya mtoto wako tumboni, usisite kuwasiliana na daktari wako. Unapofikisha wiki ya 24 ya ujauzito bila kuhisi mtoto wako akirusha mateke tumboni, bila shaka unapaswa kuwasiliana na mtaalum wa afya. Watafanya vipimo kudhibitisha kuwa mtoto wako ako salama kupitia kwa kipimo cha ultrasound.
Je, mapigo ya moyo ya mtoto tumboni huanza muda gani ikiwa hili ndilo lililokuwa swali lako kuu, ni matumaini yetu kuwa una jibu kwa sasa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Hatua Za Ukuaji Wa Mimba Na Kinachofanyika Katika Kila Trimesta