Uraibu Wa Kutoka Nje ya Ndoa Nchini Kenya

Uraibu Wa Kutoka Nje ya Ndoa Nchini Kenya

Ni kisa cha kughadhabisha baada ya nchi kuamkia habari za kuhuzunisha mwanamme mmoja alipo funga sehemu za siri za mke wake. Kumekuwa na visa vingi vya wanaume nchini Kenya kuhisi kana kwamba wanamiliki mili ya bibi zao. Kuna kesi nyingi ambapo wanaume wengi wana wachapa wanawake wao wanapo wakosea. Iwapo elimu na kuhamasishwa kwa haki za wanawake kuna tiliwa mkazo, kuna baadhi ya jamii ambapo mambo haya ya kitamaduni bado yana tokea. Ila, kisa hiki cha mume kumfunga bibi yake na glue sehemu zake nyeti ili asitoke nje ya ndoa kime kithiri mipaka. Tuna angazia marital infidelity in Kenya.

Mwanamme huyu kutoka upande wa kusini wa counti ya Kitui inasemekana kuwa aligundua kuwa bibi yake alikuwa na uhusiano na wanaume wengine wasio pungua wanne.  Aligundua haya kwa kupitia mtandao wa kijamii na bibi yake aliwaona wanaume wengine punde tu alipotoka kwenda kazini.

marital infidelity in Kenya

Ila je, nini chanzo cha tabia hii ya wanandoa kutoka nje ya ndoa nchini Kenya?: Marital  Infidelity in Kenya

Kuna baadhi ya sababu zinazo wafanya wanandoa kutoka nje ya ndoa na kuwa na uhusiano na watu wengine. Mtindo huu wa kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kume kuwa kawaida kati ya jinsia zote mbili. Na kujulikana kwa sana kama ‘mpango wa kando’. La kushangaza zaidi ni kuwa mtindo huu pia unafanyika kati ya wanandoa wazee. Wanawake wazee wana watafuta vijana wachanga wa kuwa nao na wanaume wazee pia hawaachwi nyuma. Kuna dhibitisha kupotoka kwa maadili kwenye jamii za kisasa.

Ila je, nini hasa kinacho fanya uraibu huu kuwa mwingi kiasi hiki?

  1. Mapenzi ya pesa

Kwa vijana wanao kuwa na uhusiano na watu walio kula chumvi kuwaliko, sababu ya kawaida zaidi inayo sababisha tabia hii ni kupenda pesa. Wengi wao huhusika katika mahusiano haya ili wapate pesa ya kukimu mahitaji yao. Huenda wengine wao ni uzembe wa kufanya kazi na kutafuta njia rahisi ya kupata pesa. Huenda kwa wengine ikawa ni kutumiwa na walio na pesa (being taken advantage off).

  1. Kuishi maisha ya tabaka la juu

Tunaishi kwa kipindi cha wakati ambapo watu wengi hasa vijana wachanga wanataka kuishi maisha ya tabaka la juu. Na pia kuonyesha wanarika wao kuwa maisha yao i-sawa. Jambo hili linawafanya kutafuta njia za kupata pesa bila ya kufanya kazi kuyakimu mahitaji yao. Hata kama una mpenzi wa rika lako unaye mwona, unapata kuwa wasichana wengi wana watafuta wazee ambao wataweza kuyakimu mahitaji yao ya kipesa.

  1. Kuto tosheleka

Baadhi ya watu wanao toka nje, hufanya hizi kwa kuto tosheleka na wanacho pata kutoka kwa wapenzi wao.  Unapo tarajia mwenzi wako afanye kitu ila hafanyi unacho taka, wengi badala ya kuongea na wapenzi wao, wana amua kutoka nje na kutafuta mipango ya kando ili watoshelezwe na wapate kile ambacho hawakipati wakiwa kwenye nyumba zao.

Ni muhimu kwa wanandoa kuwa na ngumzo wazi kati yao. Iwapo kuna jambo ambalo wangetaka kufanyiwa, wawajulishe wapenzi wao ili waweze kuwa tendea. Badala ya kutoka kwenda kutafuta njia ingine ya kupata wanacho tafuta. Hili litakuwa muhimu katika kuregesha mapenzi kwenye ndoa na kukabiliana na tatizo la kutoka nje ya ndoa.

marital infidelity in Kenya

  1. Mtindo ibuka

Mtindo huu wa kuwa na wapenzi wengi umetamba na huenda watu wengi wanajihusisha kwani ni jambo linalo fanywa na kila mtu. Ili kuwa kama wengine, wanajipata wakifuata uraibu huu ili wahisi kuwa wako kama marafiki zao.

Ni kweli kuwa watu wamepotoka maadili na kamwe hawa heshimu ndoa kama ilivyo kuwa hapo zamani. Hapo kale, ndoa na uhusiano uliheshimiwa na hakuna ambaye angefanya jambo la kuharibu ndoa iliyo fanywa hasa kanisani mbele ya Mungu na watu. Ila nyakati zimebadilika na kamwe watu hawatilii maanani kuishi maisha yenye heshima zake.  Kwa kupenda anasa za dunia, wasichana wengi na wavulana wanajipata katika uraibu huu ili wakimu mahitaji ya maisha ghali wanayo taka kuishi.

Hitimisho kuhusu mjadala huu

Ila ni jambo la muhimu kuwa elimisha watu kuhusu kufanya kazi kuyakimu mahitaji yao ili waishi bila ya kujiingiza katika uraibu kama huu. Pia ni muhimu hasa kwa wana ndoa kuenzi ndoa na kuwa na mazungumzo wazi. Iwapo mwenzi wako anakosea, mwambie kinacho kufurahisha na kile ambacho kinakukasirisha ili kuepuka jambo hili la kutoka nje ya ndoa.

Ni dhabiti kuwa kanisa pia ina jukumu la kuwa elimisha watu kuhusu maadili na kuheshimu ndoa na uhusiano. Tusipo fanya hivi, uraibu huu utakithiri mipaka.

marital infidelity in Kenya

Kumekuwa na visa vingi vya wachumba kuuana baada ya kupata habari kuwa mtu ambaye wana uhusiano naye anatoka nje na kufanya mapenzi na watu wengine. Tabia hii isipo komeshwa, kutakuwa na janga kubwa nchini. Ni vyema unapo jihusisha na mtu, uwaache wengine na iwapo bado unahisi kana kwamba hauko tayari, usijiingize kwenye mahusiano huku uki fahamu bayana kuwa haulitaki jambo lile.

Marital infidelity in Kenya ni jambo ambalo limekuwa kwa ongezeko kuu kwa miaka michache iliyo pita. Kisa na maana, kuvifuata vitu ambavyo sisi wenyewe hatuna uwezo wa kuvinunua. Hakuna aibu na kuishi maisha ya chini kwa sasa, borake unafanya kazi kwa juhudi na azimio la kuishi maisha bora katika siku za hapo usoni.

Wanandoa pia wajue kuwa wao ndio vyoo vya watu wachanga wanao wafuata. Wafanyacho leo ndicho nasi tunapo fika wakati na umri huo tutayaiga. Waishi maisha bora na yenye heshima zake, ili tukubaliane na tatizo hili ya marital infidelity in Kenya.

Chanzo: Indiatimes

Written by

Risper Nyakio