Kuelewa mashairi ya kitalu na umuhimu wake kwa watoto wachanga

Kuelewa mashairi ya kitalu na umuhimu wake kwa watoto wachanga

Hapo zamani, mtoto mchanga alikuwa analewa na nyanya yake ama mama mzazi. Mashairi ya kitalu yana pitishwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine na ni muhimu katika ukuwaji wa mtoto.

Kumekuwa na mabadiliko mengi katika muundo wa familia miaka kadhaa iliyo pita na mabadiliko zaidi yanaendelea kushuhudiwa. Hapo zamani, jukumu la kumchunga mtoto mchanga lilikua la mama mzazi na kupata msaada kutoka kwa wana jamii. Hivyo mtoto kwa wakati wowote ule alikuwa mikononi na kuimbiwa nyimbo za kumlaza na mashairi bora ya kitalu. Mashairi haya yalipitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Na kuridhiwa kutoka kwa nyanya hadi kwa wajukuu wake na kutoka kwa mama hadi kwa bintiye. 

Kufuatia mabadiliko mengi yaliyo tendeka katika familia, jukumu la kumchunga mtoto limetwikwa kwa mama. Iwapo mama anafanya kazi, anamuacha mtoto punde baada ya kujifungua kwani anapaswa kurudi kazini. Hana budi wala kumtafuta mfanya kazi atakaye kuwa anamchungia mtoto wakati anapo kuwa kazini. Kufuatia jambo hili, mashairi ya kitalu yana andikwa kwa vitabu. Kwani si wafanya kazi wote wanao jua njia hizi za utamaduni za kuwaimbia watoto nyimbo za kitalu. Mashairi ya kitalu yana lengo la kumsaidia mtoto.  Maneno yanayo tumika kwa mashairi ya kitalu ni yale ambayo ni rahisi kutamka na kukumbuka. Yana urudiaji mwingi unao msaidia mtoto kukumbuka. 

Watoto wachanga wanapo zaliwa, hawana uwezo wa kubagua njema na mbaya na pia uwezo wao wa kuskia bado ni mdogo. Baada ya wiki moja ama mbili, wana anza kutofautisha maneno kutoka kwa watu na sauti kutoka kwa vifaa vinginevyo. Pole pole mtu anapokuwa, anaweza kuona, kuskia na pia kunusa.

Kumwelekeza mtoto kutumia ishara anazo ona ni muhimu katika kusaidia ubongo wake kukua. Mtoto anapo ona ishara moja mara nyingi, anaiweka kwa akili na anaweza kukumbuka. Mashairi ya kitalu ni bora katika kumsaidia mtoto Kukuwa. Unapo mwambia jambo moja la kusisimua muda baada ya mwingine, anaweza kukumbuka. Mtoto anafuata unacho fanya, jambo unalo tenda na anapo endelea Kukuwa, anatamka maneno unayo yasema. Mashairi ya kitalu yametengenezwa kwa njia maalum kwa sababu ya watoto wachanga.

Mashairi bora ya kitalu yana paswa kuzingatia mambo haya

Kuelewa mashairi ya kitalu na umuhimu wake kwa watoto wachanga

Urudiaji:

Urudiaji ni muhimu kwa mtoto. Hana uwezo wa kuyaweka maneno mengi akilini wala kukumbuka kila kitu. Ila unapo tamka neno moja mara kwa mara, mtoto analiweka neno hilo akilini na pole pole anaweza kukumbuka.

 Kusisimua:

Picha na maneno yanayo kuwa kwa methali za kitalu yanapaswa kuya ya kusisimua. Picha zilizo na rangi nyingi za kuvutia zina inasa akili ya mtoto yule mchanga. Kwa hivyo anapo ona picha hizi mara nyingi, anaweza kukumbuka. Na pia kumsaidia mtoto kukuza ubunifu wake.

Maneno mafupi:

Kwani mtoto bado hajakuwa na ana shida ya kutamka maneno marefu. Ni muhimu kutumia majina mafupi. Kuepuka kumtatiza zaidi katika utamkaji wake.

Mashairi ya kitalu pia yanasaidia kumtuliza mtoto alale ama anapo lia. Yana adhari chanya kwa maisha ya mtoto na katika ukuwaji wake. Yanasaidia watoto kuwa na kamusi ya kibinafsi. Pole pole wanaweza kutofautisha kati ya maneno na maana ya kila neno. Ni muhimu pia katika kukuza ubunifu wa mtoto na kuisaidia akili yake kukua. Pia mtoto anaweza kuwasiliana na watu walio karibu naye kama vile mama na baba mzazi ama nyanya yake. Hata kama maneno anayo yatamka anapo anza si sanifu kabisa, yanaendelea kusanifika anapo endelea Kukua na kuyajua maneno tofauti. 

Mtoto anaweza kutumia ishara. Kama anapokuonyesha kitu fulani, anatumia kidole kukupa ishara. Mashairi ya kitalu yana saidia mtu mzima kumfunza mtoto mchanga maneno ya asili yake. Ni muhimu kwa watoto wenye umri wa miaka 3-5. Inasaidia mtoto kujua lugha yake asili inayo julikana kama lugha ya kwanza ama lugha ya mama. Mashairi haya pia yana andaa akili ya mtoto anapo timiza umri wa kujiunga na shule, akili yake inakuwa tayari kuanza kusoma na kujua maneno mengi zaidi. Ili kuimarisha Uwasiliano kati yako na mwanao, ni muhimu uweze kufahamu mashairi  machache ya kitalu. Unapo yasema kwa mwanao, mnakuwa na mawasiliano ya kihisia. Kwa upole mtoto anaanza kujua sauti yako unapo ongea.

Mashairi ya kitalu yana msaidia mtoto kuwa na ujuzi mwingi. Ni muhimu kwa kila mzazi aliye na mtoto mchanga ama anaye kusudia kupata mtoto kutumia mashairi ya kitalu ili kuboresha ukuwaji wa mtoto wake.

Also Read: Nigerian nursery rhymes to keep your kids entertained

Written by

Risper Nyakio