Je, Masi Rutuba Inaweza Saidia Na Kutunga Mimba?

Je, Masi Rutuba Inaweza Saidia Na Kutunga Mimba?

Matibabu ya masi ya kurutubisha ni matibabu ya upole, undani, yasiyo ingiliana na mwili ya sehemu ya tumbo yanayo saidia na mzunguko wa damu, lymph na neva kwenye sehemu ya tumbo.

Ikiwa una jaribu kutunga mimba, nafasi kubwa ni kuwa umeangalia mbinu tofauti za kuongeza nafasi zako za kuwa na mtoto. Huenda ukawa umesikia kuhusu ama kufikiria kuhusu kupata masi ya kurutubisha. Swali ni, masi inaweza kusaidia kutunga mimba kweli?

Masi ya kurutubisha ni nini hasa?

masi ya kurutubisha

Kulingana na fertilitymassage.co.uk, matibabu ya masi ya kurutubisha ni matibabu ya upole, undani, yasiyo ingiliana na mwili ya sehemu ya tumbo yanayo saidia na mzunguko wa damu, lymph na neva kwenye sehemu ya tumbo. Mbinu hii haiboreshi mzunguko wa damu tu, mbali ina leta damu freshi kwenye ovari na uterasi. Wataalum wana sema kuwa aina hii ya masi inaweza tuliza tishu zenye vidonda na kutatua fallopian tubes zilizo ziba.

Viungo vingine vinavyo faidika kutokana na masi hii ni maini, matumbo na tumbo. Lengo la masi hii ni kupunguza matatizo ya kihisia na kifizikia. Pia ina rahisisha uchafu ama mabaki magumu yaliyo kusanyika kwenye gut. Matokeo ya mwisho ni kuhisi kuwa tumbo yako iko nyepesi na haija shikana kama hapo awali.

Masi hii ina fanya kazi kivipi?

Kabla ya kuanza utaratibu huu, daktari wako atakuuliza maswali kuhusu hali ya  afya yako ya uzalishaji. Na kuwa makini kuandika historia yako ya kimatibabu na changamoto unazo pitia na ugumba. Ili kumsaidia kutayarisha masi itakayo fanya kazi vyema zaidi kwako. Kujua ujumbe kukuhusu kutasaidia kuamua wakati bora katika mzunguko wako wa kufanya utaratibu huo. Ili kubadilisha hali ya ugumba wako na kukusaidia kutunga mimba. Masi hii inafanywa kwa kutumia mikono na mtaalum wa masi.

Unapaswa kuendea masi ya kurutubisha wapi?

masi ya kurutubisha

Unapaswa kuendea huduma za mtu anaye shikilia kazi ya kupiga msi peke yake ama aliye na vyeti vya kufanya hivi. Kwani kuna watu wengi sana wanao dai kuwa weledi katika nyanja hii, ila kazi yao sio bora. Na huenda wakafanya hali yako iwe mbaya zaidi.

Masi hii inaweza tatua ugumba?

Kulingana na utafiti uliofanyika, kuna uhusiano kati ya mawazo mengi na mzunguko duni wa damu kwenye uterasi. Mzunguko duni wa damu kwenye sehemu hizi zinazo husika na uzalishaji kunaweza zuia kutunga mimba.

Vyanzo: NHS

fertilitymassage.co.uk

International Journal of Therapeutic Massage and Bodywork

US National Library of Medicine

Soma Pia: Njia Mwafaka Zaidi Za Kutunga Mimba

Written by

Risper Nyakio