Kulinganisha kusomea nyumbani na kusoma kwa jadi nchini Kenya

Kulinganisha kusomea nyumbani na kusoma kwa jadi nchini Kenya

Wazazi nchini Kenya wameanza kuzingatia kuwafunzia watoto wao nyumbani na ila sio shuleni. Tuna angalia umuhimu wa masomo haya kwa wanafunzi na kulinganisha na mfumo wa jadi.

Masomo ni muhimu sana kwa kila mtoto. Yanasaidia kuwa na maisha bora na pia kuyaelewa mambo tofauti maishani. Kuna aina mbili za masomo nchini Kenya. Wazazi kulingana na hali yao ya kimaisha na wanacho taka watoto wapate kupitia masomo, wanaweza kuchagua masomo ambayo mtoto wao atapata. Huenda ikawa masomo ya kinyumbani ambapo wana mtafutia mtoto wao mwalimu atakaye kuwa akiwafunzia nyumbani mwao. Ama masomo ya jadi ama ya shuleni, ambapo wana tafuta shule bora yenye karo ya kiwango chao cha maisha na kuwapeleka watoto wao. Iwapo masomo ya kinyumbani nchini Kenya hayajatiliwa mkazo kwa sana, na wazazi wengi bado wana wapeleka wanao shuleni. Masomo ya kinyumbani hutendeka kwa sana katika nchi za kiUlaya, nchini Kenya wazazi wengi bado hawajalifahamu jambo hili ama wana mawazo hasi kulihusu na hawako tayari kulizingatia. Kuna baadhi ya wazazi ambao wamefuatilia masomo ya kinyumbani kwa watoto wao. Idadi ya wazazi wanao taka watoto wao wasomee manyumbani mwao imeongezeka na pia watoto wanao somea nyumbani.

Tuta angazia ulinganisho katika ya masomo haya mawili nchini Kenya, ubaya na uzuri wake.

Masomo ya kinyumbani

Kulinganisha kusomea nyumbani na kusoma kwa jadi nchini Kenya

Utafiti una yapi ya kusema kuhusu masomo ya kinyumbani

Uzuri

 • Mzazi ana uwezo wa kudhibiti ambacho mwanao anasoma
 • Unaweza kuwalinda watoto wako kutokana na athari mbaya ambazo wanaweza kumbana nazo wakitoka nyumbani
 • Unaweza kuwa himiza watoto wao kuwa masomo ni mema na wala si jambo la kukasirishwa
 • Unaweza kujenga uhusiano mwema na watoto wako kwa mko nao wakati mwingi
 • Unaweza tumia msimu wa kusoma ambao una wafaa watoto wako na kufanya marekebisho panapo faa
 • Unachagua watu ambao watoto wako wana ingiliana nao

Ubaya 

 • Watoto hawana marafiki wengi kama vile wanavyo kuwa nao wakienda shuleni
 • Kwa watoto watulivu, hawatajua jinsi bora ya kuwasiliana na kukuza mawasiliano yao na watu wengine
 • Watoto wako wana ekwa kando na wengine kwani wako kwa misimu tofauti ya masomo
 • Shuleni watoto huingiliana na watu kutoka mataifa na kabila tofauti. Wanajua jinsi ya kuishi nao kwa amani, mtoto anapo somea nyumbani inakuwa vigumu kwao kuwasiliana na watu kutoka mahali tofauti
 • Mtindo huu wa masomo ni ghali

Masomo ya Jadi

Huu ndio mtindo wa masomo unao julikana kwa sana. Umekuwa ukitumika kwa miaka mingi na wazazi wengi nchini Kenya wana ufahamu na kuamini.

Uzuri

 • Una fahamika na kuaminika na serikali ya Kenya na wizara ya masomo nchini
 • Watoto wanapewa vitabu vya bure na masomo pia hawa lipishwi katika masomo ya msingi
 • Watoto wote nchini wanasoma vitabu vinavyo fanana
 • Watoto wana ingiliana na watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi kwa hivyo wanajua kuingiliana vyema
 • Watoto pia wana kuza uwezo wao wa kuwasiliana na kupata marafiki wengi zaidi
 • Watoto wanajihusisha kwa mambo zaidi isipokuwa masomo kama vile nyimbo na mazoezi

Ubaya

 • Mzazi hana wakati mwingi na mtoto wake
 • Mzazi hana uwezo wa kuchagua mtoto wake anacho soma
 • Kuna uwezekano mtoto kusoma na kuanza tabia zisizo faa kufuatia kuingiliana na watu tofauti
 • Katika shule ambazo watoto huja nyumbani wakati wa likizo peke yake, wazazi hawana muda wa kutosha kuwa funza watoto wao imani zao
 • Watoto wana adhibiwa na katika shule zingine walimu hawana huruma. Watoto wana tumia wakati mwingi wakifanya adhabu badala ya kuwa darasani

Ni muhimu sana kwa kila  mzazi kujua uzuri na ubaya wa mitindo hii miwili ya masomo. Baada ya hapo kulingana na uwezo wake, atumie mtindo utakao mfaa mtoto wake. Na cha muhimu zaidi kudhibitisha kuwa mwanawe anasoma na anapata masomo yanayo faa. Kwa watoto walio shuleni, ni muhimu kwa mzazi kuzingatia alama za mtoto wake. Mara kadha wa kadha pia anapaswa kumtembelea mtoto wake shuleni na kujua anavyo endelea na masomo yake. Ni jambo la busara kwa kila mzazi kutenga wakati wa kutosha kuongea na mtoto wake na kumfunza imani zake na kumpa moyo. Kwa wazazi ambao watoto wao wana somea nyumbani, ni muhimu kuhakikisha kuwa wanaweza kuwasiliana na watoto wengine na kutangamana nao vizuri. Wazazi hawa pia wanafaa kuhakikisha kuwa watoto wao wana jihusisha kwa mazoezi na ila si kukaa nyumbani peke yake. Pia wanaweza kuwatembeza mahali tofauti tofauti waone mazingara mapya.

Read Also: 9 Fun Learning Activities To Engage Your Preschooler

Written by

Risper Nyakio