Punde tu mama anapo gundua kuwa ana mimba, huenda akapata wasiwasi kuhusu vitu anavyo paswa kuchukua na madhara yake kwa mimba. Tazama baadhi ya maswali maarufu zaidi katika mimba!
Maswali Maarufu Katika Mimba

Kaffeini nyingi ina athari hasi kwa ujauzito. Mwanamke mwenye mimba anapaswa kupunguza kiwango cha kaffeini anacho chukua kwa siku. Sio zaidi ya vikombe viwili kwa siku.
Hatari kwa fetusi. Kuchukua kaffeini nyingi kunamweka mama katika hatari ya kupoteza mimba.
Kudhibiti kiwango cha kaffeini
Si rahisi kukoma kutumia kaffeini kwa kasi ikiwa ulikuwa umezoea hapo awali. Punguza kiwango unacho chukua kila siku. Kisha baadaye uanze kutumia kinywaji kingine badala ya kaffeini.

Mama mjamzito anapaswa kujitenga na vileo kabisa anapo kuwa na mimba. Hakuna kiwango kilicho salama katika mimba, hata kuonja kidogo. Kuna magonjwa kama vile fetal alcohol syndrome inayo husishwa na kunywa pombe katika mimba.
Hatari kwa fetusi. Vileo na pombe katika mimba vina husishwa na ulemavu wa kifizikia, kiakili na kitabia katika mtoto.
Mama anapo kunywa vileo, vinamfikia mtoto kupitia kwa placenta. Na kubaki kwenye mfumo wa mtoto kwa muda mrefu. Mfumo wake wa neva una athiriwa.
Ushauri kwa mama
Hakuna shaka unapo kunywa pombe kabla ya kufahamu hali yako ya mimba. Ila unapo jua, kuwa unatarajia, koma kunywa pombe. Ikiwa unatatizika kuwacha pombe, zungumza na mtaalum wa afya akushauri.

Kuvuta sigara katika mimba huwa na hatari nyingi kwa mtoto mchanga. Moshi ya sigara hufikia fetusi kupitia kwa placenta.
Athari kwa fetusi. Kemikali zilizoko kwenye sigara zina hatari ya kumfanya mama ajifungue kabla ya wakati, kujifungua mtoto aliye fariki ama mtoto aliye na uzani wa chini.
- Dawa zilizo nunuliwa kwa kemia
Mjamzito anapaswa kujitenga na dawa zilizo nunuliwa kwa kemia bila kushauriwa na daktari.
Hatari kwa fetusi. Kuna baadhi ya dawa ambazo huwa na athari hasi kwa fetusi. Mama asipo soma kijikaratasi kinacho andamana na dawa hizo, huenda akahatarisha maisha ya fetusi.
Mama anastahili kutumia dawa alizo shauriwa na mtaalum wa afya. Hakikisha kuwa daktari anaye kutibu anafahamu hali yako ya mimba. Ili aweze kujua dawa zitakazo kufaa na zilizo hatari kwako. Hata unapo umwa na kichwa, jizuie kununua dawa kwa duka la dawa bila kudhibitisha ikiwa ni salama kwa hali yako.
Soma Pia:Hatua 3 Za Uchungu Wa Mama Katika Mimba Na Jinsi Zinavyo Tendeka