Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Maswali Maarufu Kuhusu Mimba ya Pili na Majibu Yake

2 min read
Maswali Maarufu Kuhusu Mimba ya Pili na Majibu YakeMaswali Maarufu Kuhusu Mimba ya Pili na Majibu Yake

Kujua baadhi ya maswali maarufu kuhusu mimba ya pili na majibu yake kunawasaidia wanawake kujipanga katika safari hii mpya.

Tofauti na siku za hapo awali ambapo wanandoa wangepata watoto wengi, mambo ni tofauti hivi sasa. Mara nyingi watu wanapoingia kwenye ndoa, tayari washapanga nambari ya watoto ambao wangependa kupata kwa majaliwa. Kwa wanandoa wanaolenga kupata watoto wawili, huenda wakawa tayari mwaka mmoja baada ya kupata kifungua mimba. Tuna angazia baadhi ya maswali maarufu kuhusu mimba wa pili ambayo wanandoa huenda wakawa nayo.

Maswali maarufu kuhusu mimba ya pili

  1. Ugonjwa wa asubuhi

maswali maarufu kuhusu mimba ya pili

Ikiwa nilikuwa na ugonjwa wa asubuhi ulionisumbua kwa sana mara ya kwanza, nitataabika na hali hiyo tena?

Kulingana na wataalum wa afya, wanawake walio tatizika na ugonjwa wa asubuhi mara ya kwanza, watapata ugonjwa wa asubuhi tena. Mara ya kwanza, hata ugonjwa wa asubuhi ulipokuwa mwingi, ungeweza kupumzika. Sasa hivi, itakuwa migumu kwani ungali una mtoto mwingine unayemtunza.

2. Mwendo wa fetusi

maswali maarufu kuhusu mimba ya pili

Katika ujauzito wa kwanza, fetusi hukaa kabla ya mama kuanza kuhisi mwendo wa fetusi kwenye uterasi. Katika mimba ya pili, utaanza kuhisi mwenda wa fetusi mapema katika safari yako ya mimba. Pia, mimba itaanza kuonekana mapema ikilinganishwa na mimba ya kwanza.

3. Mazoezi katika mimba

maswali maarufu kuhusu mimba ya pili

Kufanya mazoezi katika mimba ya pili kutanitatiza?

Katika mimba ya kawaida isiyo na matatizo, mama aliye na mimba yake ya pili anaweza kufanya mazoezi. Kuinua kifungua mimba chake pia hakuna shaka. Hata hivyo, ni vyema kuwa makini kuhakikisha kuwa hautajiumiza katika mambo haya.

4. Uzito wa mwili

maswali maarufu kuhusu mimba ya pili

Je, nitaongeza uzito sana katika mimba ya pili?

Kwa wanawake wanaofanya mazoezi, nafasi kubwa ni kuwa huwa hawaongezi uzito sana katika mimba. Hata baada ya kujifungua, huwa rahisi kwao kupunguza uzito waliopata katika safari yao ya mimba.

5. Kunyonyesha kifungua mimba changu kutaathiri mimba?

kutoa gesi tumboni kwa mtoto mchanga

Napaswa kuendelea kumnyonyesha mtoto hata baada ya kupata mimba?

Maziwa ya mama hayapunguki anapokuwa na mimba. Ila, mimba yake inapoendelea kukua, huenda maziwa ya mama yakabadili yanavyoonja. Kwa sababu hii, watoto wengi huanzia kula mama zao wanapokuwa na mimba.

Mbali na maswali haya maarufu kuhusu mimba ya pili, mama hapaswi kuwa na hofu zozote. Lishe yenye afya ni muhimu katika kipindi hiki kuhakikisha kuwa fetusi inapata virutubisho tosha na kudumisha ukuaji wa mwili wa mama.

Soma Pia: Maswali 7 Maarufu Kuhusu Ngono Katika Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Maswali Maarufu Kuhusu Mimba ya Pili na Majibu Yake
Share:
  • Je, Kulala Kwa Mgongo Katika Mimba Kuna Athari Hasi Kwa Mama na Mtoto?

    Je, Kulala Kwa Mgongo Katika Mimba Kuna Athari Hasi Kwa Mama na Mtoto?

  • Matatizo Katika Trimesta ya Tatu Utakayoshuhudia

    Matatizo Katika Trimesta ya Tatu Utakayoshuhudia

  • Je, Anita Nderu Ana Mimba?

    Je, Anita Nderu Ana Mimba?

  • Je, Kulala Kwa Mgongo Katika Mimba Kuna Athari Hasi Kwa Mama na Mtoto?

    Je, Kulala Kwa Mgongo Katika Mimba Kuna Athari Hasi Kwa Mama na Mtoto?

  • Matatizo Katika Trimesta ya Tatu Utakayoshuhudia

    Matatizo Katika Trimesta ya Tatu Utakayoshuhudia

  • Je, Anita Nderu Ana Mimba?

    Je, Anita Nderu Ana Mimba?

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it