Mwanamke anapopata mimba kwa mara ya kwanza huwa na maswali mengi kuhusu mimba. Tuna angazia maswali maarufu kuhusu ngono katika mimba.
Maswali maarufu kuhusu ngono katika mimba

- Je, kufanya mapenzi katika ujauzito ni salama?
Ikiwa mama ana mimba ya salama isiyokuwa na matatizo yoyote ya kiafya. Kufanya mapenzi ni salama na hakumuweki katika hatari zozote katika kipindi hiki. Ikiwa mwanamke atahisi uchungu usiopungua ama kuvuja damu baada ya kufanya tendo la ndoa, ni muhimu kuwasiliana na daktari wa afya ya kike anayemshughulikia.
2. Kufanya mapenzi kutamwumiza mtoto?
Kufanya ngono katika mimba hakuna athari hasi kwa mtoto. Kumbuka kuwa fetusi huwa imezingirwa na maji ya amniotic yanayomlinda kutokana na hatari zozote. Mtoto kwenye uterasi ako salama.
3. Ujauzito huathiri hamu ya tendo la ndoa katika mimba
Hamu ya kufanya tendo la ndoa katika mimba hubadilika katika kila muhula na huwa tofauti kwa wanawake wote. Huku wengine wakipata hamu iliyoongezeka ya kufanya tendo la ndoa, wengine hukosa hamu. Katika muhula wa kwanza, mama husumbuliwa sana na kichefuchefu na huenda akakosa hamu ya kufanya mapenzi. Kisha ikrejelea katika trimesta ya pili na kupungua katika trimesta ya tatu kufuatia kukosa starehe kunako fuatia ongezeko la tumbo na uzito wa mwili.
4. Mitindo bora ya kufanya ngono katika ujauzito ni ipi?
Katika ujauzito, mama hushauriwa kutumia mitindo inayompa starehe, bila kujishinikiza. Katika trimesta ya kwanza, mitindo kama missionary na cowgirl. Mtindo wa cowgirl ambapo mwanamke huwa juu humsaidia kudhibiti uzito wake na kiwango cha kupenya katika tendo la ndoa. Ni muhimu kwa wanandoa kujaribu mitindo tofauti hadi watakapopata inayowafaa zaidi.

5. Ni wakati upi ngono sio salama katika ujauzito?
Kulingana na mimba ya mama, kuna wakati ambapo daktari anaweza kuwashauri wanandoa kutofanya mapenzi. Hizi ni baadhi ya sababu zinazoweza kuwafanya wanandoa kushauriwa wajitenge na tendo la ndoa katika mimba.
Ikiwa mama ana historia ya kujifungua kabla ya wakati, ana tatizo la placenta previa, kuvuja damu, ana mimba ya watoto mapacha ama zaidi ama ikiwa maji ya amniotic yana vuja.
6. Ngono inaweza kusababisha uchungu wa uzazi usikomaa
Kufanya ngono katika mimba hakuwezi sababisha uchungu wa uzazi usiokomaa. Isipokuwa pale ambapo daktari anatangaza mimba kuwa katika hatari ya uchungu wa uzazi usiokomaa.
7. Ni lazima kufanya ngono katika mimba?
Sio jambo la lazima, huenda mama akakosa hamu ama kuwa na ujauzito usio salama na kushauriwa na daktari kujitenga na tendo la wanandoa.
Kufanya tendo la ndoa hudumisha utangamano kati ya wanandoa. Kwa wanandoa wasioweza kufanya tendo hili katika mimba kufuatia matatizo tofauti, wanaweza kudumisha uhusiano wao kwa njia zingine za mapenzi kama kukumbatiana, kuwa pamoja kwa muda, kufanya kazi za kinyumbani pamoja ama kwa kumpa mchumba masi.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Dalili 11 Za Mimba Ya Mtoto Msichana Za Kuangazia