Maswali 5 Katika Uhusiano Unayo Ogopa Kumwuliza Bwana Yako Lakini Unastahili

Maswali 5 Katika Uhusiano Unayo Ogopa Kumwuliza Bwana Yako Lakini Unastahili

Hakuna haja ya kufanya mapenzi ikiwa hamuwezi jadili kwa uwazi mambo yanayo husika na kufanya mapenzi.

Kuuliza maswali yanayo husika katika uhusiano wenu ni mojawapo ya njia za kuhakikisha kuwa mna mazungumzo wazi na ni njia ya kuhakikisha kuwa mna utangamano wa kudumu. Kuna baadhi ya mada ambazo huenda ukahisi hofu ama kuona haya kuanzisha katika uhusiano wako na mchumba wako. Lakini maswali haya ni muhimu sana kwani yana kujuza zaidi kuhusu mpenzi wako na uhusiano mlio nao. Kwa hivyo usione haya kuuliza maswali haya. Pia yana saidia kuondoa siri zozote katika uhusiano wenu.

Tume orodhesha maswali muhimu ambayo unapaswa kumwuliza mwenzi wako. Unamjua mwenzi wako zaidi, kwa hivyo tafuta njia isiyo na makali ya kumwuliza maswali haya.

Maswali 5 Katika Uhusiano Unayo Paswa Kumwuliza Mchumba Wako

wanawake kutoka nje ya ndoa

  1. Je, natimiza malengo yako kitandani?

Hata kama mada ya kufanya mapenzi huepukwa sana, ni muhimu sana katika uhusiano. Na hakuna haja ya kufanya mapenzi ikiwa hamuwezi jadili kwa uwazi mambo yanayo husika na kufanya mapenzi. Haijalishi wakati ambapo mmekuwa pamoja na mchumba wako, ni vyema kujadili mambo haya. Na kamwe usione aibu kumwuliza matumaini yake kitandani na ikiwa unamtosheleza. Kwa kufanya hivi, mtaweza kuongea mambo mnayo yatamani na jinsi ya kuyatimiza.

2. Napiku viwango vya mchumba wako wa awali

Huenda ikaonekana kama una masuala ya kuto jiamini ama kama ungependa kujua zaidi kuhusu uhusiano wao wa hapo awali. Bila shaka kila mtu hasa mwanamke anataka kujua kuwa yeye ni bora kuliko mchumba wako wa hapo awali.

3. Umetoka nje ya uhusiano wetu ama kuhisi haja ya kupata mchumba mwingine?

Maswali 5 Katika Uhusiano Unayo Ogopa Kumwuliza Bwana Yako Lakini Unastahilikutoka nje katika ndoa

Kutoka nje ama kutafuta mchumba mwingine unapo kuwa katika uhusiano kamwe hakukubaliki. Kutoka nje sio rahisi na huenda ukahisi kuwa una majukumu mengi. Kutoka nje ya ndoa na kuhisi haja ya kutoka nje ni masuala tofauti. Na kuwa na mazungumzo haya kutawasaidia kutatua masuala na sababu zinazo kufanya uhisi haja ya kutoka nje.

4. Mna onana na mchumba wako wa awali

Ni vigumu kufikiria kuwa mtu unaye mpenda na kumdhamini huenda akawa bado ana mpenda na kumthamini mchumba wake wa hapo awali. Na bila shaka utavunjwa moyo kufahamu kuwa mwenzi wako bado ana hisia za mchumba wake wa hapo awali, lakini afadhali kujua ukweli kuliko kuishi gizani.

5. Una furaha kuwa nami?

Kuuliza swali hili hakumaanishi kuwa hauna imani na mchumba wako. La hasha, kuuliza swali hili kutakusaidia kujua ikiwa kuna mambo zaidi ambayo mchumba wako angependa mfanye pamoja ili mhisi furaha.

Tuna fahamu kuwa maswali haya sio rahisi kuuliza. Lakini nini gumu zaidi, kufahamu ukweli ama kutojua ukweli kisha kulia baadaye?

Soma Pia: Sababu Kwa Nini Mchumba Wako Atatoka Nje Ya Ndoa Yenu

Written by

Risper Nyakio