Maswali 5 Ya Kimapenzi Unayo Aibika Kumwuliza Bwana Yako... Ila Ni Sawa!

Maswali 5 Ya Kimapenzi Unayo Aibika Kumwuliza Bwana Yako... Ila Ni Sawa!

Baadhi ya maswali ambayo ungependa kumwuliza mchumba wako ila una aibika kufanya hivyo. Uko huru kuongeza maswali zaidi ambayo ungependa kuuliza.

Kuuliza maswali ya uhusiano wenu ni njia ya kuboresha mazungumzo yenu na kudumisha utangamano wenu katika uhusiano huo. Kuna aina fulani ya mada ambazo huenda ikawa vigumu kuanzisha katika mazungumzo yenu na mchumba wako, ila, baadhi ya maswali yana paswa kuulizwa.

maswali ya uhusiano-wanandoa

Tume orodhesha maswali haya na ni sawa ikiwa utafikiria mara mbili kabla ya kumwuliza mchumba wako, lakini utatafuta ujasiri wa kumwuliza.

Maswali 5 Ya Uhusiano Unayo Hitaji Ujasiri Kuuliza

1. Je, nakutosheleza kitandani?

relationship questions

 

Maswali ya mahitaji ya kingono huwa mada ambazo hazi zungumziwi kwa uwazi. Haijalishi ikiwa mmekuwa kwa uhusiano kwa wiki chache ama miongo mingi. Unataka kuhakikisha kuwa unatimiza majukumu yako ya kitandani vyema na kumtosheleza mchumba wako. Lakini huenda ikawa ngumu kwa watu wengi kuuliza swali hili kwa sababu unaweza umia sana kutambua haumtoshelezi mchumba wako. Walakini, maisha yenu ya kimapenzi yanaweza jengwa na kuboreshwa na wakati.

2. Je, mimi ni mzuri kuliko wachumba wako wa awali?

maswali ya uhusiano-wanandoa

Swali nyingine ambayo huenda ikawa na utata kuuliza mchumba wako ni ikiwa unaweza kushindana na uhusiano wake wa hapo awali. Bila shaka ungependa kufikiria kuwa mchumba wako anakuthamini zaidi ya alivyo wathamini wachumba wake wa hapo awali. Lakini huwezi jua kwa kweli hadi uulize. Hii ndiyo sababu kwa nini ni swali ngumu kwa watu kuuliza.

3. Je, umewahi kutoka nje ya uhusiano wetu na unahisi haja ya kufanya hivyo?

maswali ya uhusiano- wanandoa

 

Kutoka nje ya uhusiano na kuwa na mpenzi wa kando ni vigumu na pia ni kitendo ambacho kitamwumiza mchumba wako kihisia. Huenda kitendo hiki kikasababisha vurugu na utengano kati yenu. Mara nyingi swali hili huhisi kana kwamba ni mtego. Kulingana na watu walio kwenye uhusiano, swali hili huenda lika boresha ama kuharibu uhusiano wenu. Kitendo cha kutoka nje ya uhusiano ni tofauti na kuhisi haja ya kutoka nje na hata kama mawili haya ni tofauti, yote yana madhara hasi.

4. Bado unahisia za kimapenzi kwa mchumba wako wa hapo awali?

maswali ya uhusiano - wanandoa

 

Ni vigumu kufikiria kuwa mchumba wako unaye mpenda na kumthamini kwa sana bado ana hisia za kimapenzi kwa mchumba wake walio wachana. Hutaki kuonekana kana kwamba una shindana na wapenzi wake wa hapo awali, lakini hili ni swali ambalo watu wengi huwa nalo. Kufahamu ikiwa kuna kitu wanacho paswa kuwa na shaka kuhusu wachumba wao na wapenzi wao wa hapo awali.

5. Una furaha kuwa nami?

maswali ya uhusiano- wanandoa

Kuto kuwa salama katika uhusiano huenda kukatutatiza ndani kwa ndani. Na mojawapo ya njia bora za kutatua shaka hizi ni kuuliza majibu kutoka kwa vyanzo vyetu  vya nje. Huenda ukahisi hauko salama kuhusu mahali pako katika uhusiano na ukahitaji mchumba wako kukuhakikishia na kukukumbusha thamani yako.

Maswali haya hata kama huenda ukapuuza haja ya kumwuliza mchumba wako, yana umuhimu. Ikiwa ungependa kuwa na uhusiano ulio wazi kumwongelesha mchumba wako kuhusu kitu chochote, hii ni njia mojawapo ya kuboresha mazungumzo yenu na pia kukuza uhusiano wenu.

Tafuta siku moja mnapo kuwa mmepumzika, unaweza fanya uamuzi wa kumpeleka mahali pa kustarehe. Baada ya kula chakula ama kunywa kinywaji, tafuta ujasiri ndani yako kisha umwulize maswali haya.

Sio jambo gumu na una uwezo wa kulifanya!

Wall Street Journal

Soma pia: Is he husband material? Qualities of a good husband

 

Written by

Risper Nyakio