Mazungumzo ni muhimu katika kila kitu. Ili ndoa iwe na ufanisi, ni muhimu kwa wanandoa kujifunza jinsi ya kuzungumza wanavyohisi. Kuzungumzia hisia zako na vile ambavyo ungependa kudhaminiwa sio jambo rahisi. Na hakuna anaye penda kurudia jambo moja kwa muda mrefu. Lakini, sio mambo makubwa yanayo anzisha matatizo, ni vitu vidogo vidogo vinavyo sababisha matatizo haya. Kuna sababu nyingi zinazo ibua matatizo katika ndoa. Lakini wanandoa wanapo zifahamu na kuzitatua, ndoa yao itakuwa sawa.
Kipi kinacho sababisha matatizo katika ndoa na unaweza kutatua kivipi?

- Hisia kubatilishwa
Baada ya siku ndefu kazini, untarajiwa kuwa unapomwelezea mchumba wako kilichofanyika, atakusikiliza kisha kukuegemeza kihisia. Lakini unapomweleza kisha anyamaze ama akose kuhisi ulivyo tarajia, hisia zako zitaumizwa.
Hata kama sio jambo kubwa, hautahisi vyema mchumba wako anapopuuza hisia zako. Atahisi kana kwamba hapendwi. Huenda akafanya kitu sawa wakati ujao ili kuhakikisha kuwa mchumba wake anahisi alivyo hisi wakati ambapo hisia zake zilipuuzwa.
Kutatua: Msikilize mchumba wako, kisha umwambie kuwa unaelewa alichokipitia. Hata kama huenda ukakosa kukubaliana naye. Cha muhimu zaidi ni kuwasikiliza.
2. Kutosema unachotaka
Kutosema unachotaka kutakufanya uumie katika ndoa. Ni vigumu kwa mchumba wako kutojua hasa unachokitaka.
Kutatua: Unapo taka kitu, mweleze, anapofanya jambo lisilo kufurahisha, kuwa na mazungumzo ya kina naye. Mazungumzo haya wakati wote hayatakuwa ya kufurahisha, mbali huenda kukawa na hisia za chuki katika mazungumzo haya. Lakini mchumba wako ataelewa unachotaka na mwishowe mtakuwa na maisha bora.
3. Kuto tenga muda wa kuwa pamoja
Familia huwa na mambo mengi yanayochukua muda mwingi. Kulea watoto, kufanya majukumu ya kinyumbani baada ya siku ndefu kazini, na kudumisha uhusiano na mchumba wako. Katika wakati mmoja, wanandoa hufahamu kuwa hawana muda tosha wa kuwa pamoja.
Kutatua: Ni muhimu kwa wanandoa kutenga muda angalau mara moja kwa wiki, kuwa pamoja na kuzungumza kuhusu maisha yao mbali na watoto. Kufanya hivi kunasaidia kudumisha uhusiano uliokuwa kabla ya watoto.

4. Sio mashindano
Wanandoa wanaoshindana katika kila kitu huwa vigumu kufurahishana kwani mmoja wakati wote anajaribu kuwa bora kuliko mwingine. Hakuna mshindi katika ndoa, na kufanya hivi husababisha kuvunjika kwa ndoa.
Kutatua: Ndoa yenye afya ni kufikiria kama timu moja na kufanya mambo yenu kama timu. Kumaanisha kuwa, unafanya juhudi kumhusisha mchumba wako katika uamuzi wako.
5. Mapenzi ya kifizikia kufifia
Mambo yanayo sababisha mazungumzo kufeli katika ndoa pia husababisha kuharibika kwa maisha ya kimapenzi ya wanandoa. Kukosa kufanya mapenzi huenda kukawafanya wanandoa wengine kutengana.
Kutatua: Msikilize mchumba wako na utimize mahitaji yake ya kifizikia, kiakili na kihisia. Tenga muda wa kuwa pamoja.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Dalili Za Mimba Ya Mwezi Mmoja Baada Ya Kufanya Tendo La Ndoa!