Matatizo Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba Na Wakati Wa Kuenda Hospitalini

Matatizo Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba Na Wakati Wa Kuenda Hospitalini

Joto jingi mwilini unapo kuwa na mimba, zaidi ya digri 38, huenda ika ashiria kuwa mama ana maambukizo ambayo ni hatari kwa afya ya mama na mtoto.

Kwanza, hongera kwa kutunga mimba! Baada ya miezi tisa, matumaini yako ya kuitwa mama yata timia na utapatana na kitita chako cha furaha. Ikiwa ni kifungua mimba chako, utakuwa na hisia nyingi, zitakazo andamana na maswali yasiyo koma kuhusu unavyo paswa kufanya mambo tofauti. Wakati unapo paswa kuwa na shaka na ikiwa baadhi ya mambo yatakayo tendeka ni kawaida katika safari ya mimba. Hata kama mimba yako itakuwa yenye afya na isiyo na matatizo, kuna baadhi ya ishara unazo hitajika kuwa makini nazo katika miezi ya kwanza ya ujauzito wako. Huenda yaka ashiria matatizo katika trimesta yako ya kwanza ya mimba. Kumbuka kuwa kipindi hiki ni nyeti sana na unapaswa kujitunza kadri uwezavyo. Unapo ona jambo unalo shuku sio la kawaida, wasiliana na daktari wako kutoa shaka zozote zile.

Matatizo katika trimesta ya kwanza ya ujauzito

kutapika katika mimba

  1. Kutapika sana na kichefu chefu wakati wote

Ni kawaida kwa wanawake wengi walio wajawazito kuwa na kichefu chefu na kutapika katika trimesta ya kwanza. Huku wengine wakishuhudia dalili hizi katika safari yote ya ujauzito. Lakini ikiwa unatapika sana, kiasi kuwa hauwezi weka chakula ulichokula tumboni, ni vyema kuwasiliana na daktari wako.

2. Kuvuja damu

Kuvuja kiasi kidogo cha damu huenda kukawa kawaida, ama kitu cha kuto kutia kiwewe. Ila, unapogundua kuwa una vuja damu kwa sana, kiasi cha kujaza pedi, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako bila kukawia. Huenda hii ikawa ni ishara ya mimba ya ectopic, ama kuharibika kwa mimba. Unapo enda hospitalini, utafanyiwa kipimo cha damu na ultrasound kubainisha kinacho fanyika mwilini mwako. Kutoka hapo daktari wako atakueleza ikiwa umepoteza mimba ama unacho stahili kufanya.

3. Joto jingi mwilini

Joto jingi mwilini unapo kuwa na mimba, zaidi ya digri 38, huenda ika ashiria kuwa mama ana maambukizo. Maambukizo ni hatari kwa afya ya mama na mtoto. Unapo ripoti kuhisi hivi, hakikisha una mweleza daktari wako ishara zingine zinazo andamana na hali hii, kama vile matatizo ya kupumua ama kuumwa na mwili.

4. Uchungu unapo enda msalani

dalili za mapema za mimba

Kuhisi uchungu unapo enda haja ndogo ni ishara ya maambukizo katika mfumo wako wa mkojo. Yasipo tibiwa, huenda ukapata maradhi hatari ama hata uchungu wa uzazi usiokomaa na kujifungua kabla ya wakati.

Soma Pia: Jinsi Ya Kufahamu Kubanwa Kwa Ujauzito Kwa Kweli

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio