Safari ya ujauzito inakaribia kufika tamati. Lakini kabla ya kupatana na mtoto wako, kuna changamoto chache zinazokuwa katika muhula huu wa mwisho. Matatizo katika trimesta ya tatu utakayoshuhudia ni kama vile kukosa usingizi, kuenda msalani mara kwa mara na kuvimba.
Matatizo Maarufu Katika Trimesta ya Tatu

- Kuvimba
Katika wiki ya 30 ya ujauzito, miguu huanza kufura, hasa kufuatia uzito wa zaidi wa mtoto. Miguu na vifundo vya miguu huvimba kufuatia uzito mwingi unaoshinikiza upande wa chini wa mwili.
Njia za kukabiliana na tatizo hili ni:
- Kuto simama kwa muda mrefu
- Kufanya mazoezi
- Kuwekelea miguu kwenye kiti unapokaa chini
- Kuvalia viatu ambavyo havikufinyi
2. Kukosa usingizi
Tatizo la kukosa usingizi huwa maarufu katika trimesta ya tatu. Mabadiliko ya homoni mwilini hasa ongezeko la progesterone mwilini huchangia pakubwa katika suala hili. Kuhisi haja ya kwenda msalani mara kwa mara hata usiku huathiri mfumo wa kulala.
Jinsi ya kukabiliana na tatizo hili:
- Lala kwa upande mmoja, wa kulia ama kushoto
- Tumia mto kukuwezesha kupata starehe kidogo unapolala
- Koga kabla ya kulala, tazama vidokezo zaidi hapa

3. Maumivu ya mgongo
Ongezeko la homoni ya progesterone katika mimba hutuliza misuli na viungo ili kustahimili mimba inayokua na kuboresha uwezo wa mwendo wa pelviki ili mtoto aweze kupita kwenye kanali ya kujifungua kwa urahisi zaidi.
Suluhu:
- Koga kwa maji moto
- Tumia pedi yenye joto kwenye mgongo kutuliza uchungu
- Kufanyiwa masi mara kwa mara kutuliza uchungu na kusaidia kupumzika
4. Kushiba mbio
Katika trimesta ya tatu, huwa vigumu kula chakula kingi kama ilivyokuwa hapo awali. Kadri uterasi inavyozidi kukua, ndivyo inavyosukuma tumbo, na kufanya nafasi ya chakula kupunguka.
Kukabiliana na suala hili:
- Kula chakula kidogo mara tano kwa siku
- Kula chakula kisicho na kalori nyingi
- Epuka kula chakula chenye pilipili nyingi
- Ongeza maziwa ya bururu kwenye lishe yako
5. Kuhisi kizunguzungu
Kusimama kwa muda mrefu kutaleta hisia ya kizunguzungu.
Suluhu:
- Simama kwa upole
- Kuto simama kwa muda mrefu
- Tembea mara kwa mara
- Uchungu kwenye maziwa

6. Maumivu kwenye maziwa
Maumivu kwenye maziwa katika mimba husababishwa na homoni mwilini.
Suluhu:
- Nunua sindiria zinazotosha kwani saizi imeongezeka
7. Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Kuhisi haja ya kwenda msalani mara kwa mara ndiyo sehemu inayosumbua zaidi katika muhula wa tatu wa mimba. Kibofu kimefinywa na kwa hivyo kuibua haja ya kwenda msalani kila mara.
Hakuna mengi unayoweza kufanya kuhusu jambo hili.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Orodha ya Watu Mashuhuri Nchini Kenya Walio na Mimba