Utafiti: Wanawake Wenye Wanaume Wa Kuvutia Huwa Na Nafasi Zaidi Za Mitindo Ya Lishe Isiyo Ya Afya

Utafiti: Wanawake Wenye Wanaume Wa Kuvutia Huwa Na Nafasi Zaidi Za Mitindo Ya Lishe Isiyo Ya Afya

Kulingana na utafiti, wanawake walio na mabwana wa kuvutia wamepatikana kuwa na hatari zaidi za kupata matatizo ya kula chakula kisicho na afya.

Bibi anapo ulizwa kuhusu hasara za kuwa na bwana wa kuvutia, huenda ukajibu kwa laini za kuto hisi salama, na kuwa wana hofia bwana yao kutoka nje ya ndoa. Lakini kuna jambo ambalo huenda hauja sikia hapo awali: utafiti umegundua kuwa walio na mabwana wa kuvutia wamepatikana kuwa na hatari zaidi za kupata matatizo ya kula chakula kisicho na afya.

Kulingana na utafiti katika chuo kikuu cha Florida State University, kuwa na mpenzi anaye vutia haku sababishi matatizo ya kula tu, mbali kuna weza tatiza afya ya kiakili ya mwanamke. Ikiwa mwanamke anajiona kuto pendeza ikilinganishwa na mpenzi wake, kuna hatari za kuwa na mitindo ya kula isiyo ya kiafya.

Kivipi? Kwanza, bibi ya bwana wa kuvutia alianza kuwa makini zaidi na uzito wake, na kumpa shinikizo la kuhesabu kalori, kula mara kwa mara na hata katika kesi zingine, kuanzisha kutapika.

"Tuki elewa jinsi uhusiano wa mwanamke unavyo athiri uamuzi wake wa lishe na hatari za kijamii za kuwa na tabia za kula zisizo za kiafya, tutaweza kuwaelewa," mtafiti Tania Reynolds alisema katika kauli iliyo tumwa kwa Medical Daily.

Reynolds na timu yake wali afikia mapato haya kwa kuokota ujumbe kutoka kwa wanandoa 113 walio kuwa wamefunga pingu za maisha sio wakati mrefu ulio pita. Na ambao walikuwa kwa umri wao wa miaka ya ishirini. Wali angalia kiwango cha kuvutia kwa kutumia ripoti ama ujumbe kutoka kwa wanafunzi wa chuo kikuu wa jinsia na kabila tofauti.

Matatizo ya kula ni nini?

matatizo ya kula

Kulingana na EatingDisorders.org, kutatizika kula ni tofauti na matatizo ya kula, lakini kuna ashiria aina tofauti za ulaji usio wa kawaida, kama vile kula chakula tofauti kilicho karibu nawe, kuhesabu kalori kuliko sisitizwa zaidi, na kulazimisha kutapika.

Ni kidogo zaidi kuliko matatizo ya kula, walisema Psychology Today, kwa sababu wanao tatizika na ulaji ulio tatizika hawa jihusishi katika mitindo ya kula isiyo yenye afya kama kawaida kama walio na matatizo ya kula.

Unawezaje msaidia bibi yako ikiwa ana tatizika na ulaji ulio tatizika?

Ikiwa una shuku kuwa bibi yako ana tatizika na hali hii, ni muhimu kujua kuwa hai athiri afya yake ya kifizikia tu mbali ya kiakili pia. Mhakikishie urembo wake na umuhimu wake. Kuangalia zaidi ya anavyo kaa kifizikia ni muhimu, kusherehekea nguvu zake na mambo yote mazuri anayo keta maishani mwako.

Kuwa mvumilivu, usichoke kutosheleza njaa na kiu yake ya kusifiwa na kumwonyesha mapenzi kumsaidia kupigana dhidi ya matatizo hatari ya kula.

Vyanzo: Medical Daily, Psychology Today, EatingDisorder.org

Soma PiaLishe Na Siha Ya Mama Mwenye Mimba: Vyakula Muhimu Katika Mimba

Written by

Risper Nyakio