Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)

3 min read
Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)

Ulezi wa siku hizi una kabiliana na changamoto nyingi kufuatia mabadiliko katika mitindo ya maisha na teknolojia. Tazama baadhi ya matatizo ya ulezi.

Mbinu za ulezi za siku hizi zimebadilika sana zikilinganishwa na mbinu za wavyele wetu. Matatizo ya ulezi ni mengi kufuatia mabadiliko ya kiteknolojia na mitindo ya maisha. Enzi za kale, wanaume walienda kufanya kazi kuzitafutia familia zao lishe. Huku wanawake wakibaki nyuma kuwalea watoto, kuchunga familia na kufanya kazi za kinyumbani.

Majukumu yamebadilika kwa sana katika kitengo cha familia. Waume kwa wanawake wote wanafanya kazi ili kupata kipato cha kukidhi mahitaji ya familia zao. Gharama ya maisha imepanda ikilinganishwa na hapo awali na lazima wanandoa wasaidiane katika kukidhi mahitaji ya familia zao. Watoto hawapati wakati mwingi na wazazi wao kwani kila mara wako mbioni kutafuta kazi na pesa. Kiwango cha wanawake wanao baki nyumbani kuichunga familia na kuwalea watoto ni kidogo sana. Ni kazi nyingi kusawasisha wakati wa kuwa na familia na kutafuta kazi, na kufanya matatizo ya ulezi kuwa mengi. Baadhi ya changamoto za ulezi wa kisasa ni zipi?

Matatizo ya ulezi

matatizo ya ulezi

  1. Kukosa wasaa wa kutosha

Mojawapo ya matatizo makuu yanayo kumba ulezi ni kukosa wasaa tosha wa kuwa na watoto wako. Kati ya masaa 24 katika kila siku, mzazi ana jukumu la kufanya mambo mengi na bado kuwa na wakati wa kuwa na watoto wake. Hasa kwa familia ambapo hakuna mfanya kazi, inakuwa vigumu kwa mzazi kupata wakati wake wa kipekee.

Watoto wanahitaji wakati wao pamoja na wazazi wao na wasipo pata, inakuwa ni vigumu kwa mzazi kujua kinacho endelea maishani mwao. Na wako katika hatari ya kumea pembe na kuto wasikiza wazazi wao.

2. Utumizi mkubwa wa teknolojia na mitandao ya kijamii

Teknolojia ina faida nyingi na imesaidia pakubwa katika kufanya vitu kama mawasiliano yawe rahisi na kuimarisha kiwango cha huduma za afya na kadhalika. Ila kila chenye upande hasi kina upande chanya. Siku hizi, watoto wengi wanapata simu na kuwa na mitandao ya kijamii katika umri mchanga. Kutumia wakati mwingi kwenye mitandao ya kijamii kunachangia kwa sana katika kupotoka kwa maadili katika watoto. Hawafuati wanacho ambiwa na wazazi wao, mbali wanataka kuwa kama watoto wengine na kuiga wanacho ona. Kwa hivyo wazazi wasipo tenga wakati tosha wa kuwa na watoto wao, huenda wakakosa maadili.

matatizo ya ulezi

3. Mabadiliko ya kifamilia

Sio jambo nadra kuwa kati ya familia kumi, tano zina mzazi mmoja. Familia za mzazi mmoja zimeshuhudia ongezeko kubwa. Mzazi huyu ametwikwa jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa familia yake haikosi mahitaji ya kijumla. Kati ya kutafuta kipato kizuri cha kuridhisha mahitaji ya kimasomo, chakula, mavazi na mahali pa kulala, mzazi hana wakati tosha wa kuwa na watoto wake.

Licha ya matatizo ya ulezi kuwa chungu nzima, mzazi anastahili kujaribu kadri awezavyo kuhakikisha kuwa anapata wakati wa kuzungumza na watoto wake kila siku. Kwa kufanya hivi, anapunguza hatari ya watoto kupotoka njia na kukosa nidhamu, na pia kuwasaidia kufuzu masomoni.

Chanzo: healthline

Soma Pia: Ratiba Ya Chakula Cha Wiki Moja Cha Familia Yako

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)
Share:
  • Changamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana Nayo

    Changamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana Nayo

  • Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

    Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

  • Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

    Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

  • Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

    Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

  • Changamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana Nayo

    Changamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana Nayo

  • Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

    Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

  • Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

    Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

  • Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

    Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it