Kila uchao watoto wanazidi kuzaliwa. Huonekana jambo la urahisi na kweli si ngumu ikizingatiwa huchukua muda wa masaa machache kujaliwa mtoto. Ila safari nyingine na iliyo ndefu huwa imeng’oa nanga. Nayo ni safari ya ulezi. Kuna matatizo ya ulezi ama safari huwa laini?
Matatizo Ya Ulezi

Wazazi wanapopata habari kuwa ni wajawazito hujawa na furaha nyingi. Na mara tu wanaanza kujiami kwa maarifa kuhusu watoto. Jinsi ya kuwaosha, kuwatunza, chakula na pia mavazi. Maarifa juu ya chanjo na habari nyingine tofauti. Hili ni kwa kuwa kila mzazi hutaka kumpa mtoto wake maisha mazuri ila huwa kuna matatizo ya ulezi ata baada ya kujiami kwa maarifa.
Haya matatizo ni kama vile:
Wazazi wengi wanapotarajia mtoto huwa hawana fursa au mwanya wa kuzungumzia magonjwa. Hii ni ikibainika wazi kuwa kila mtoto anapoanza safari yake duniani atakubana na magonjwa. Hili huwa kwa vile bado mwili wake hauna kinga dhabiti. Lakini pindi wanavyokua huweza kukabiliana na magonjwa itakikanavyo.

Mtoto huja na mahitaji mengi ya kifedha. Wakati mwingine kama wazazi hupuuzilia wakidhani bado mtoto ni mdogo mpaka anapowasili na kuelewa ata kabla waanze shule bado mahitaji ni mengi. Kutokuwa na fedha za kutosha inafanya hii safari kuwa ngumu. Kutoka mavazi, mahitaji ya hospitali na mahitaji mengine kama tundua.
Wazazi wengi huwa wamezoea maisha yao kuwa na utaratibu fulani wakiwa na masaa ya kutosha ya kulala. Ila mtoto anapofika wengi bado huwa hawajajitayarisha kwa mabadiliko. Mtoto huhitaji masaa mengi na mzazi ambalo huchosha. Pia wakati watu wanafaa kulala mtoto anaweza kuwa ameeamka ambalo linamaanisha mzazi hawana wakati tosha wa kupumzika.
Kuna watoto ambao huzaliwa wakiwa na ulemavu wa aina fulani. Wazazi wengi katu hawatapanga kuwa na huu uwezekano ilihali hutokea kila mara. Huku kutokuwa na nafasi ya hili kutokea huwapa wazazi changamoto. Hii ni kwa kuwa huyu mtoto atahitaji mambo ya kitofauti ikilinganishwa na mtoto aliye mzima. Hili litakuwa changamoto kwa wazazi wowote wale.
Kila ujio wa mtoto unamaanisha mabadiliko kwa maisha ya mama ama mzazi yote. Kila kitu katika maisha ya familia hubadilika kwa kuwasili kwa mtoto. Kazi na majukumu mengine hufiki kikomo kwanza kumpa nafasi yule mdogo. Kujiandaa vilivyo kwa kumpokea mtoto kutaweza kukusaidia kukabiliana na matatizo ya ulezi ambayo yanaweza kuchipuka wakati wowote.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Wazazi Kuchoka Katika Ulezi, Ishara Na Vyanzo Vyake