Kufanya uamuzi wa kuanzia familia huambatana na jukumu kubwa la kujitayarisha vilivyo. Kimawazo, kifizikia na kifedha pia. Tazama baadhi ya matayarisho kabla ya kupata mimba ambayo mama anapaswa kufanya.

- Fahamu historia ya kimatibabu ya familia yenu
Kujielimisha kuhusu historia ya kimatibabu ya familia yenu ni jambo muhimu kabla ya kuanza harakati za kushika ujauzito. Japokuwa na jambo linalo puuzwa sana, lina manufaa mengi kwa wazazi. Zungumza na wazazi wako kuhusu magonjwa ya kupitilizwa kati ya vizazi. Mwulize kuhusu safari yake ya ujauzito ilivyokuwa na changamoto alizokumbana nazo. Zungumza na wanawake wengine katika familia kutoka pande zote mbili, ya mama na baba. Ni muhimu kwa wanandoa kufanyiwa vipimo kabla ya kutunga mimba.
2. Koma kutumia mbinu za uzazi wa mpango
Jambo la kawaida sivyo? La hasha, hili sio jambo la kawaida, huenda mwanamke aliyeweka IUD kusahau kuwa anayo. Ni vyema kukumbuka kukoma kutumia mbinu za kupanga uzazi unapojaribu kupata mimba. Ni vyema wakati wowote kuzungumza na daktari kuhusu njia bora ya kukoma kutumia uzazi wa mpango. Kumbuka kuwa, mwili huchukua muda kabla ya kurejelea utendaji kazi wa kawaida baada ya kukoma kupanga uzazi.
3. Hakikisha una fedha tosha

Safari ya ujauzito huwa na gharama nyingi. Ni vyema kwa wanandoa kuhakikisha kuwa wana fedha tosha kukimu mahitaji yanayo andamana na mimba. Gharama kama za kliniki, kununua mavazi mapya, kununua mavazi ya mtoto na kadhalika. Panga fedha za kukimu mahitaji ya baada ya kujifungua, kwa kufanya hivi, wanandoa wana muda wa miezi tisa kutafuta pesa zaidi iwapo kitita cha fedha walichotenga cha baada ya kujifungua hakitoshi.
4. Jitenge na sumu
Epuka kukaa kwenye mazingira yaliyo na sumu, kuwa na viwango vingi vya sumu mwilini kutatatiza juhudi zako za kutunga mimba. Baadhi ya sumu mbali iliyoko kwenye mazingira ni kama vile pombe na sigara. Kuna baadhi ya bidhaa za utunzaji wa ngozi zilizo na sumu, na ni hatari kwa afya ya mwanamke. Ni vyema kuwa makini na bidhaa unazotumia mwilini.
5. Fanya mazoezi
Mazoezi yanafaida nyingi kwa mama kabla, anapokuwa na mimba na baada ya kujifungua. Mama anayefanya mazoezi kabla na anapokuwa na mimba mara nyingi huwa hatatiziki na kufura miguu ama kuumwa na mgongo kwa sana. Baada ya kujifungua, mama aliyekuwa akifanya mazoezi hupunguza uzito wa mwili kwa kasi. Mazoezi ni baadhi ya matayarisho kabla ya kupata mimba yaliyo muhimu zaidi.
Soma Pia: Kuharibika Kwa Mimba Na Umuhimu Wa Kusafisha Mji Wa Uzazi