Mama Hakikisha Kuwa Umeangazia Vitu Hivi Kabla Ya Kupata Mimba!

Mama Hakikisha Kuwa Umeangazia Vitu Hivi Kabla Ya Kupata Mimba!

Mazoezi kwa mama anaye kusudia kupata mimba ni muhimu sana kwani yanasaidia kuupa mwili wako nguvu itakayo hitajika katika safari ya ujauzito.

Tofauti na hapo awali ambapo wanandoa walipata watoto bila kuwapangia, mambo hivi sasa yamebadilika sana. Katika siku za kale, wanandoa waliamini kuwa watoto ni utajiri na kadri ulivyo kuwa na wengi ndivyo ulivyo kuwa tajiri. Pia, watoto hawa wangewasaidia wazazi wao kufanya kazi za kinyumbani na kuwatunza walipo zeeka. Siku hizi, watoto wamekuwa gharama kubwa. Na wanandoa wanachukua muda kujipanga vyema ili kuhakikisha kuwa wanatosheleza mahitaji ya watoto wao. Na kupata watoto ambao wataweza kuwalea bila matatizo. Tazama matayarisho ya kupata mimba!

Kuna mambo muhimu ya kufanya hasa kwa mama kabla ya kupata mimba: Matayarisho ya kupata mimba

matayarisho ya kupata mimba

  • Kuwa na mazungumzo wazi na mchumba wako

Uamuzi wa kupata mtoto haupaswi kuwa wa mtu mmoja tu, ila ni muhimu kwa wanandoa wote wawili kuwa na mawasiliano wazi. Nyote wawili mtagharamia mtoto, kifedha na kihisia kwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa nyote mko tayari kuwa na mwanafamilia mwingine.

  • Wasiliana na daktari wako

Hii ndiyo mojawapo ya hatua za kwanza katika kupata mimba. Kabla kujitosa kwenye juhudi za kuanza kutafuta mtoto, mwanamke na mwanamme wanapaswa kuwasiliana na daktari wao. Ili wafanyiwe vipimo vinavyo stahili kudhibitisha iwapo afya yao iko sawa na kama mmoja wao ana matatizo yoyote ya uzalishaji. Daktari wenu atawashauri vitu mnavyo paswa kufanya ili kurahisha mchakato wa kutunga mimba kwa urahisi.

  • Angalia hali yako ya kifedha

Watoto wana mahitaji mengi ya kifedha, hata kabla ya kujifungua, mama anahitaji kuanza kula lishe bora na kwenda kliniki, zote ambazo zinahitaji fedha. Anapo enda kujifungua pia, kuna kiasi cha pesa kinacho hitajika kulingana na anavyo jifungua, njia asili ama kupitia upasuaji wa c-section. Ni vyema kuhakikisha kuwa una pesa tosha za kukimu mahitaji ya mwanao.

matayarisho ya kupata mimba

  • Ongeza mazoezi kwenye ratiba yako

Kufanya mazoezi sio muhimu kwa wanao jaribu kukata uzani zaidi tu, ila pia kwa wanawake wanao jaribu kutunga mimba. Mazoezi yanasaidia kuupa mwili wako nguvu itakayo hitajika katika safari ya ujauzito. Pia, yana kinda dhidi ya ongezeko kubwa la uzito wa mwili.

  • Tupilia mbali utumiaji wa dawa za kulevya

Afya bora ni muhimu sana kwa mama anaye jaribu kutunga mimba. Kwa sababu hii, ana stahili kuhakikisha kuwa amekoma kutumia dawa za kulevya, sigara na vileo. Kwani vitu hivi vitapunguza nafasi zake za kutunga mimba kwa urahisi ama kutatiza mchakato wa kujaribu kutunga mimba.

Soma PiaJinsi Ya Kufurahia Mapenzi Baada Ya Kujifungua Kupitia Upasuaji Wa C-section

Written by

Risper Nyakio