Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua

Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua

Ikiwa una hisi kuwa una uwoga wa uchungu wa uzazi, wasiliana na mama kanda wako aje akukande mara ya mwisho kabla ya kuenda hospitalini kujifungua.

Imekuwa safari ndefu ya miezi tisa. Ya kusisimua, kusoma mengi na yenye changamoto zake. Na baada ya miezi tisa ama nane na wiki mbili, muda wa kumkaribisha mtoto umewasili. Ni mambo gani mama anapaswa kuwa makini nayo katika matayarisho ya mwisho kabla ya kujifungua?

Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Kujifungua

matayarisho ya kujifungua

  • Begi la kujifungua

Kwa sasa, begi la mama la uzazi linapaswa kuwa tayari. Mavazi ya mtoto na mahitaji wakati wa kujifungua na baada, mavazi ya mama na mahitaji mengine. Ili kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa na kimewekwa kwenye begi la uzazi la kujifungua, mama anastahili kumwuliza daktari anapo enda kliniki ya mwisho vitu anavyo paswa kubeba anapo enda kujifungua. Ili kuepuka kuwacha mahitaji muhimu nyumbani unapo enda hospitalini. Mara kwa mara, hakikisha kuwa kila kitu kinacho hitajika kiko kwenye begi hiyo.

  • Dalili za uchungu wa uzazi

Kufahamu dalili za uchungu wa uzazi ni muhimu sana katika matayarisho ya mwisho kabla ya kujifungua. Kwani utaweza kujua wakati unapo stahili kuanza kufunga safari kuelekea hospitalini. Hakikisha kuwa una mtu mwingine karibu nawe, kama vile mwanafamilia, mchumba wako ama rafiki wako wa ndani atakaye kupeleka hospitalini. Ni vigumu kwa mama kuendesha gari katika hali hii.

  • Mlinzi wa watoto

matayarisho ya kujifungua

Kwa mama aliye na watoto wengine, ni vyema kuwa na mipango kabambe ya utakaye achia watoto wako. Kama hauna mfanya kazi, wasiliana na mmojawapo wa wanafamilia wako ili akusaidie kuwachunga watoto wako unapo enda kujifungua. Nunua mahitaji ya nyumba kama vyakula na vitu vya kutumia ili kuhakikisha kuwa watoto wako hawakosi kitu chochote unapo enda hospitalini. Watayarishe kimawazo kuwa utarudi na mtoto mwingine na watakuwa na ndugu mwingine. Ili pia wafahamu kuwa hautakuwa nyumbani kwa siku kadhaa.

  • Masi kabla ya kujifungua

Ikiwa una hisi kuwa una uwoga wa uchungu wa uzazi, wasiliana na mama kanda wako aje akukande mara ya mwisho kabla ya kuenda hospitalini kujifungua. Kwa njia hii, misuli mwilini mwako itatulia, mawazo kupunguka, uchungu kupungua na pia utaweza kulala vyema.

Kumbuka kuto kuwa na uwoga wa kujifungua. Hata kama sio jambo rahisi, ila, pia lita pita. Kama Africaparent, tunakutakia mema unapo enda kumkaribisha mwanao!

Soma Pia: Kuna Uwezekano Wa Mama Kupata Mimba Katika Umri Wa Ugumba?

Written by

Risper Nyakio