Kwa kawaida, kujifungua ni jambo kuu ambalo hubadilisha maisha ya mama na pia familia kwa ujumla. Hivyo matayarisho kabla ya huu wakati huwa ni ya lazima. Hii ni kama vile ya kisaikolojia na kiakili lakini haikomi hapo. Matayarisho ya upasuaji wa C-section pia husaidia kukinga kutokana na dharura zinazoweza kupatikana.
Matayarisho Ya Upasuaji Wa C-Section

Katika kipindi kabla ya uchungu wa uzazi kutokea kila mama hujua njia yake ya kujifungua. Ila hali tofauti za kiafya zinaweza kusababisha kubadilika kwa njia moja hadi nyingine. Kujifungua kwa njia ya upasuaji ni salama kwa mama na mtoto, ila ni upasuaji mkubwa.
Hivyo basi inashauriwa isichukuliwe kwa urahisi. Matayarisho ya upasuaji wa C-Section ni ya muhimu. Haya matayarisho sio lazima ianze siku chache kabla ya kujifungua, mbali inafaa kuwa safari ya matayarisho pindi mama anapokuwa mjamzito.
Jambo la kwanza ni kuhudhuria klinki. Klinki huwa sio muhimu tu kabla ya kujifungua mbali pia baada ya kujifungua kwa manufaa mbalimbali kama vile:
- Husaidia kutambua dalili za hatari kwa mapema
- Hueleza juu ya njia bora ya kujifungua
- Hutambua na kuzuia matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha hatari kwa mama mara anapojifungua
- Mama anapata mafunzo juu ya tarehe ya matarajio, njia ya kujifungua na pia mahali pa kujifungulia
- Hupata mafunzo juu ya dalili za hatari za ujauzito kama vile kuumwa na kichwa, kutokwa na damu ukeni na pia kizunguzungu
Maandalizi Ya Kibinafsi

Ingawa shughuli za kujifungua huwa bure katika hospitali nyingi za serikali, upasuaji sio bure. Kufanya maandalizi ya kifedha kwani mtoto huja na mahitaji mengi ni busara. Pia itakuwa muda mrefu kabla ya mtu kurejelea kazi zake za kiuchumi. Kuna mambo ya dharura yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifungua na kugharimu pesa.
Mama anafaa kuandaa njia ya usafiri ya kumpeleka hospitali na pia kumrejesha nyumbani. Hii ni kwa kuwa uchungu wa mtoto unaweza kutokea wakati wowote. Sio jambo la busara kuanza kutafuta usafiri huo wakati.
Mama mjamzito anafaa kuandaa mavazi yake na ya mtoto atakayezaliwa. Hizi ni pamoja na soksi, babyshow, pampers, kofia na whipers. Nguo za mtoto hazifai kuwa mpya lakini zifuliwe kabla na ziwe zimekauka vizuri ili mtoto asije akawa mgonjwa.
Ingawa lishe bora ni jambo la kuzingatia muda wote wa ujauzito, ata ni jukumu kubwa baada ya kujifungua. Hii husaidia kuharakisha kupona na pia kuhakikisha kuwa mama ana maziwa ya kutosheleza mtoto. Kufanya maandalizi ya vyakula na lishe au ratiba husaidia kupunguza kazi ambazo mama atahitaji kufanya baada ya kujifungua.
Haitawezekana mama aliyejifungua kurejelea kazi zingine mara moja. Matayarisho ya upasuaji wa c-section itakuwa pamoja na kutafuta mtu wa kumshughulikia kwa wakati kabla ya kupata nguvu ya kufanya kazi. Huyu anaweza kuwa Jamaa iwapo wako karibu ama mfanyikazi.
Mjamzito hushauriwa kuandamana na mtu ama Jamii hadi hospitalini. Msaidizi huwa wa umuhimu kumsaidia mama hospitalini na pia iwapo jambo la dharura litatokea.
Matayarisho ya upasuaji wa c-section haina kikomo ila kuna yale makuu kama tulivyonakiri hapa juu. Hii orodha ni tosha kuhakikisha kuwa safari yako kabla na baada ya kujifungua ni rahisi.
Soma Pia: Upasuji Wa C-section: Vidokezo Vya Kupona Kwa Kasi