Mavazi Ya Ankara Ya Kupendeza Ya Mama Mjamzito

Mavazi Ya Ankara Ya Kupendeza Ya Mama Mjamzito

Suala linalo ibuka mama anapo kuwa mjamzito ni jinsi ya kuvalia mavazi ya mitindo mipya isiyo mdhibiti kwa sababu tumbo lake linakua. Na pia vazi lenye uhuru wa kwenda kazini na kufanya shughuli zake za kila siku kwa urahisi. Tumbo linalo zidi kukua mara nyingi huenda likafanya iwe vigumu kwake kuvalia kitu chochote kinacho m-bana kwenye tumbo. Ni vyema kwa mama mjamzito kutavuta mavazi yanayo mfaa na kuendelea kupendeza hata anapokuwa na kiumbe kinacho kua tumboni mwake. Mojawapo ya njia bora zaidi za kuhakikisha hivi ni kwa kufanya mipango ya mavazi atakayo valia katika safari yake ya mimba. Makala haya yana angazia maternity dresses in ghana ili uweze kupata mawazo ya mavazi yatakayo kufaa katika kipindi hiki.

Jambo la maana ni kuwa na starehe na kupendeza wakati sawa. Njia gani bora ya kuvutia na kuwa na uhuru wako ila kumpelekea fundi wako wa mavazi kitambaa cha ankara?  Fundi wako wa mavazi anachukua vipimo vyako na kukupa nafasi tosha kwenye tumbo yako ili nguo hizi zisi kufinye.

Picha za mavazi ya ankara ya mama mjamzito

Siku zimepita ambapo wanawake walikuwa wanavalia mavazi marefu ili kuficha hali yao ya mimba. Ama kuacha kupendeza kwa sababu tumbo yao ina kua. Orodha yetu ya maternity dresses in ghana itakusaidia kuvutia ukimtarajia mtoto wako.

maternity dresses in ghana

  • Gauni ya ankara isiyo na mikono. Vazi la aina hii linakupatia uhuru katika hatua yoyote ile ya safari yako ya mimba na kukufanya upendeze. Unaweza valia na mshipi mwembamba juu ya tumbo yako ili kukupa umbo zaidi.
  • Gauni la kitambaa chenye machapisho tofauti na mikono mipana. Vazi hili linakufanya uonekane wa kipekee na unaweza livalia kwenda ofisini ama sherehe nyingine ya kirasmi. Ni bora kwa siku ambapo hakuna jua kali.

maternity dresses in ghana

  • Rinda refu maarufu kwa kimombo kama maxi. Vazi hili linakubana sehemu ya kifua na kuwa pana kwenye tumbo yako hadi chini. Pia, vazi hili halionyeshi tumbo yako sana.

Mavazi Ya Ankara Ya Kupendeza Ya Mama Mjamzito

  • Rinda la Dashiki. Dashiki haivaliwi kwenda harusini tu. Pia unaweza valia ukiwa mjamzito. Bila shaka utapendeza kwa vazi hili.

Mavazi Ya Ankara Ya Kupendeza Ya Mama MjamzitoMavazi Ya Ankara Ya Kupendeza Ya Mama Mjamzito

Mavazi ya maternity dresses in ghana yasiyo rasmi

peplum top for pregnant woman

  • Blausi ya ankara ya peplum ni bora katika kipindi hiki. Unaweza ivalia na sketi ama kaptura. Kulingana na hali ya anga ilivyo siku hiyo.

Mavazi Ya Ankara Ya Kupendeza Ya Mama Mjamzito

  • Rinda la umbo la kengele linaweza kuwa vazi ya ujauzito. Lakini usilivalie na mshipi. Ni rahisi kuvalia rinda hili na utawapendeza wengi.

Mavazi Ya Ankara Ya Kupendeza Ya Mama Mjamzito

 

  • Rinda ama blausi ya off-shoulder. Rinda la aina hii lina nafasi tosha kutengeneza rinda la ujauzito. Ukipenda pia unaweza litengeneza liwe na mifuko.

Hitimisho

Jaribu kuchanganya rangi zinazo ng'aa kwenye mavazi hayo. Ili kufanya maisha yako yang'ae pia. Epuka kuvalia rangi nyeusi.

Chanzo: Fashion Ghana

Soma pia:Lishe Ya Ujauzito: Ratiba Ya Chakula Cha Ujauzito Cha Nigeria

Written by

Risper Nyakio