Vidonda vya uterasi vya fibroids ni maarufu. Vidonda hivi vinakua hasa katika sehemu ya uterasi katika wanawake. Kuna baadhi ya watu wanao tumia matibabu asili na vyakula kupunguza athari za vidonda hivi vya fibroids. Tuna angazia zaidi iwapo mbinu hizi zinasaidia katika kupunguza athari za vidonda hivi. Tazama matibabu asili ya fibroids.
Mara nyingi, huenda mwanamke akakosa kufahamu kuwa ana fibroids hata. Kwani sio vidonda vyote vinavyo kuwa na athari, huenda sio vyote vinavyo hitaji matibabu. Kumbuka kuwa mwanamke anaweza ishi na vidonda hivi bila kugundua na bila matatizo yoyote ya kiafya. Watu wanao athiriwa zaidi ni wanawake chini ya miaka 50.
Dalili za kuwa na fibroids ni kama vile:

- Upungufu wa maji ya kuchakata chakula mwilini
- Hedhi nzito na chungu
- Kuenda haja ndogo mara kwa mara
- Kuhisi uchungu wakati wa tendo la ndoa
- Maumivu makali ya mgongo
Matibabu asili kuponya fibroids
Mara nyingi, fibroids huisha bila matibabu yoyote. Lakini ikiwa vidonda hivi vina dalili kali, daktari ana weza mshauri mwanamke kutumia matibabu kama vile tembe za kudhibiti uzalishaji ama kufanyiwa upasuaji ili kutoa vidonda hivyo.
Hata kama kuna baadhi ya matibabu ambayo yanaweza kupunguza vidonda hivi, huenda wakati mwingine mwanamke akapata athari hasi.
Jukumu la lishe bora katika kutibu fibroids

Huku utafiti zaidi ukizidi kufanyika katika nyanja hii. Kuna somo linalo dhibitisha kuwa baadhi ya vyakula huenda vika punguza hatari ya kupata vidonda vya fibroids. Huku vingine vikiongeza hatari ya mwanamke kupata fibroids.
Ulaji wa nyama
Utafiti una dokeza kuwa watu wanao kula nyama kwa wingi na chakula kilicho na kalori nyingi wako katika hatari ya kuugua vidonda hivi. Aina ya nyama nyekundu, ufuta na sukari nyingi sio nzuri. Badala yake, ni vyema kuchukua nyama nyeupe kama vile kuku ama protini za mimea.
Ulaji wa vitamini
Ulaji wa vyakula vyenye vitamini hasa A vime dhihirishwa kupunguza hatari ya mwanamke kupata fibroids. Vitamini A inapatikana kwenye vyakula kama:
- Samaki kama vile tuna na salmon
- Mboga za kijani kama mchicha
- Soya
- Ndimu na limau
- Berries
Unywaji wa vileo
Kulingana na utafiti ulio fanyika katika mwaka wa 2004, fibroids zilihusishwa na utumiaji wa vileo. Kumbuka kuwa, huku ni kuhusishwa tu, ila hakuna ushahidi kuwa vileo vina sababisha vidonda hivi.
Wanawake wana shauriwa kunywa chai ya kijani iliyo na antioxidants. Ni mojawapo ya matibabu asili ya fibroids, na ina punguza shinikizo la oxidants mwilini ambacho ni chanzo kikubwa cha mawazo mwilini. Chai hii inapunguza athari za fibroids mwilini.
Soma Pia: Kutofautisha Ute Wa Kawaida Kwa Wanawake Na Wa Mimba