Chloroquine Phosphate Dawa Iliyo Na Ufanisi Wa Matibabu Ya Homa Ya Korona

Chloroquine Phosphate Dawa Iliyo Na Ufanisi Wa Matibabu Ya Homa Ya Korona

Dunia inapo kimbililia kutafuta suluhisho kuhusu maambukizo ya homa ya korona, inaonekana kana kwamba watafiti wa Uchina huenda wakawa na suluhisho chanya!

Hapa kuna habari njema kuhusu maambukizo ya COVID-19. Wataalum wame thibitisha kuwa Chloroquine Phosphate, ambayo ni dawa dhidi ya malaria, imedhihirika kuwa na athari katika kukumbana na mambukizo haya. Kulingana na ripoti katika The Star, Sun Yanrong, mdogo wa mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Uchina cha Maendeleo ya Kifundi ya Biolojia chini ya Wizara ya Kisayansi na Kiteknologia. Alisema wataalum walikubaliana kuwa dawa ile ilipaswa kuhusishwa kwenye matibabu yanayo fuata ya homa ya korona.

Kutoka wakati ambapo kuibuka kwa majaribio ya kikliniki dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 yalihusisha matumizi ya dawa nyingi dhidi ya virusi (antiviral). Choloroquine Phosphate, na Favipiravir na Remdesivir zilichaguliwa baada ya uchunguzi mwingi,

coronavirus treatment

Chanzo cha picha: The Star

Matibabu Yamkini Ya Homa Ya Korona: Chloroquine Phosphate

Kulingana na Sun, Chloroquine Phosphate imekuwa muhimu sana kwa majaribio ya kliniki kwa hospitali zaidi ya 10 huko Beijing. Pia katika Uchina ya kusini mkoa wa Guangdong na Uchina ya katikati mkoa wa Hunan. Wagonjwa katika majaribio walionyesha kuimarika kwema katika pande tofauti za ugonjwa huu ikilinganishwa na makundi tofauti. Joto jingi ilipunguka na kulikuwa na kuimarika kwenye michoro ya CT ya mafua na wakati wa kupona ulipunguka.

Sun pia alipeana mfano wa jinsi mgonjwa wa miaka 54 huko Beijing alichukua dawa hii kwa muda wa wiki moja, baadaye alilazwa hospitalini akionyesha dalili. Baada ya wiki, viashiria vili imarika na kipimo chake kikatokea kikiwa hasi.

Kwa kuongeza, Sun alisema hakukuwa na mabadiliko ya mahututi yaliyo husishwa na dawa ile.

coronavirus treatment

Picha: Pixabay

Kulingana na Zhang Xinmin, ambaya ni mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Uchina cha Maendeleo ya Kifundi ya Biolojia chini ya wizara ya Sayansi na Kifundi, watafiti walikagua zaidi ya madawa 70,000 ama bidhaa kwa kupitia kompyuta na vipimo vya in vitro enzyme activity. Na watu waliochaguliwa 5,000 wa kutumiwa kupima dawa hizi. Dawa hizi zinapimwa katika kiwango cha cellular dhidi ya virusi vya homa ya korona. Na kuhusu madawa 100 yalichaguliwa ili kufanya utafiti zaidi yaliyo saidia kuchagua dawa za mwisho za majaribio ya kliniki.

Chloroquine Phosphate Dawa Iliyo Na Ufanisi Wa Matibabu Ya Homa Ya Korona

Chanzo cha picha: pixabay

Sehemu tofauti duniani kote, watafiti na kampuni za madawa zinaendelea kukuza  chanjo na madawa ya kukabiliana na virusi hivi.

Originally written by Syreeta

Translated by Risper

Soma Pia: Cameroonian Man Is The First African To Survive The Coronavirus In China

Written by

Risper Nyakio