Matibabu Ya Homa Kwa Watoto Ambayo Unaweza Tengenezea Nyumbani

Matibabu Ya Homa Kwa Watoto Ambayo Unaweza Tengenezea Nyumbani

Matibabu haya yata kusaidia kuponya homa watoto wako wanapo ugua.

Homa ni maambukizi ya mfumo wa kupumua. Ina sababishwa na virusi vinavyo sambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine. Homa ya watoto ni homa inayo washika watoto. Watoto wanapokuwa na homa, wanahisi vibaya na huenda wakashindwa kufanya baadhi ya vitu. Wakati mwingi, wao huanza kuhisi vibaya siku mbili baada ya kukumbana na virusi vya homa. Huenda wakawa na ishara hizi: joto jingi, kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kukosa hamu ya kula, kukohoa, kuumwa na koo. Watoto walio na homa huenda wakaanza kuchemua mara kwa mara na kutoa kamasi ama wakakaa wagonjwa. Ni vyema kwa kila mzazi kujua matibabu ya homa ya kinyumbani ambayo anaweza watengenezea watoto wake wakiugua virusi hivi. Lakini una shauriwa kumwona daktari virusi hivi vikiongezeka.

Matibabu ya nyumbani ya homa

Homa ya watoto inaweza tibiwa nyumbani, kwa kuwapa watoto wako vinywaji vingi na kuhakikisha kuwa wanapata usingizi na mapumziko tosha. Pia, hakikisha kuwa mtoto wako anakunywa acetaminophen ama ibuprofen kutuliza uchungu ama kupunguza maumivu. Usiwape watoto wako aspirin kwa sababu ina husishwa na Reye Syndrome.

Watoto wanao ugua homa wanapaswa kubaki nyumbani na wasiende shuleni hadi pale wanapo hisi vizuri. Wanapaswa kurudi shuleni baada ya joto kupungua baada ya angalau masaa 24 bila kuwapa dawa za kupunguza joto mwilini. Baadhi ya watoto wanapaswa kubaki nyumbani kwa muda mrefu. Mwuliza daktari wako ni nini nzuri kwa mtoto wako.

Baadhi ya vyakula husaidia watoto kupigana dhidi ya homa, kupona mbio na kuhakikisha kuwa kinga yao ya mwili iko juu. Kama vile maziwa ya bururu, viazi vitamu, nyama ya ng'ombe ama nguruwe na supu ya kuku.

Pia, tumeongeza matayarisho ya kinywaji kitakacho wasaidia watoto wako kupona.

matibabu ya homa

Maziwa ya turmeric

Maziwa ya turmeric yana sifika kwa kuwa matibabu ya homa, kikohozi na koo. Kinywaji hiki kina tengenezwa kwa kutumia turmeric ambayo ni kiungo chenye matumizi mengi ya kiafya. Poda ya turmeric na maziwa yana changanywa na huwa bora kwa kikohozi na homa kwani yana wingi wa antioxidants.

Tahadhari za kuangazia unapo tengeneza maziwa ya turmeric ya watoto wachanga:
 • Maziwa haya ya turmeric yanaweza tumika kwa watoto wa umri zaidi ya mwaka mmoja.
 • Unapo mwanzishia mtoto wako maziwa ya turmeric kwa mara ya kwanza, anza na kiwango kidogo.
 • Wakati wote hakikisha kuwa unatumia poda ya turmeric iliyo safi kutengeneza maziwa ya turmeric.
 • Unaweza mpea mtoto wako maziwa ya turmeric mara moja baada ya wiki mbili ama wakati anapo dhihirisha dalili za homa.
 • Maziwa ya turmeric ni nzuri kwa siku kukinyesha ama msimu wa harmattan. Ila viwango vidogo vya maziwa ya turmeric vina weza chukuliwa wakati wowote mtoto anapokuwa na dalili za kuwa na homa.

Maagizo

Wakati wa kutayarisha : dakika 15              wakati wa kupika : dakika 5            wakati wote: dakika 20

VIUNGO
 • Maziwa - Vikombe 1.5
 • Poda ya turmeric  - kijiko ⅛
 • Pilipili nyeusi - kijiko ¼
 • Sukari - vijiko 2
MAAGIZO
 1. Weka viungo vyote tayari. Chukua maziwa uweke kwenye sufuria kisha uongeze poda ya turmeric, sukari na poda ya pilipili. Kisha uchanganye vizuri.
 2. Chemsha maziwa kwa moto wa kiasi kidogo.
 3. Weka kwa glasi.

matibabu ya homa

Kuepuka homa katika watoto

Hakuna njia iliyo bainika ya kuepuka kuto pata homa. Ila kuna hatua ambazo zinaweza kusaidia kupunguza kusambaza kwa homa:

 • Wafunze watoto wako kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni.
 • Waonye dhidi ya kuchukua tishu zilizo tumika.
 • Wafunze kuto tumia vikombe na sahani zilizo tumika.
 • Waeke watoto nyumbani iwapo wana homa.
 • Iwapo hawana tishu, wakohoe ama kuchemua kwa upande wa ndani wa mkono wao.

Matibabu Ya Homa Kwa Watoto Ambayo Unaweza Tengenezea Nyumbani

Je, unawasaidia watoto wako vipi wasipate homa wanapokuwa nyumbani? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi.

Chanzo: Kidshealth

Soma pia: Food Poisoning In Kids: All You Need To Know To Keep Your Kids Safe

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio