Matibabu Ya Kichefu Chefu Kwa Mama Mwenye Mimba

Matibabu Ya Kichefu Chefu Kwa Mama Mwenye Mimba

Wanasayansi bado hawaja dhibitisha jinsi hasa B6 huwa na athari kwa kichefu chefu, lakini huenda ika husika na jinsi inavyo chakata amino acids na kusaidia kupunguza neurotransmitters.

Mama, huenda ukawa unatatizika na kuhisi kichefu chefu na ugonjwa wa asubuhi katika mimba, na kushangaa kwanini yote haya yana tendeka. Na iwapo kuna matibabu ya kichefu chefu katika mimba. Tuna elewa unayo yapitia. Hisia za kutapika ambazo huwezi dhibiti ni mojawapo ya hisia zinazo kera zaidi katika kipindi hiki.

Walakini, kichefu chefu katika mimba ni kawaida sana na ni kawaida. Na kama kauli hii ita kufanya uhisi vyema, kutapika katika mimba ni ishara kuwa homoni zako za mimba zina fanya kazi vyema.

Kipi kinacho sababisha kichefu chefu katika mimba?

kutapika katika mimba

Kuhisi kutapika katika mimba kuna sababishwa na viwango vya juu vya homoni za mimba. Inaonyesha kuwa homoni ya human chorionic gonadotrophin (HCG) inatolewa katika viwango vya juu.

HCG ndiyo homoni inayo hakikisha kuwa mtoto anapata virutubisho tosha kutoka mwilini wako, hasa katika wiki za kwanza. Homoni zingine zinazo weza kusababisha kichefu chefu katika mimba ni oestrogen na homoni za fikira nyingi kama cortisol. Kukosekana kwa virutubisho kama vile vitamin B6, huenda ikawa ni sababu zingine.

Habari njema ni kuwa kichefu chefu katika ujauzito haki hatarishi mtoto. Wamama wengi huanza kuhisi vyema baada ya trimesta ya kwanza (karibu wiki ya 12-14). Wamama wachache hushuhudia ishara katika trimesta ya pili. Na wasio na bahati sana hushuhudia kichefu chefu katika safari yao yote ya ujauzito.

Baadhi ya wamama hushuhudia kichefu chefu kingi, hali inayo fahamika kama hyperemesis gravidarum (HG), ambapo wana tatizika kuto toa hata maji. Hali hii inaweza sababisha kukosa maji tosha mwilini na kupoteza uzito wa mwili na kukuwacha bila virutubisho tosha. Kwa hivyo, ni vyema kuwasiliana na daktari kasi iwezekanavyo.

Matibabu ya kichefu chefu: Vidokezo vya kujitunza

Mama, kutatizika na kuhisi kichefu chefu huenda kukaonekana kama njia ya kawaida ya kuanza safari yako ya ujauzito, lakini usiwe na shaka. Mabadiliko haya rahisi katika mtindo wako wa maisha na vidokezo vya kujitunza huenda vika kusaidia katika kupunguza kichefu chefu katika mimba:

 • Kula chakula kidogo, mara kwa mara

kichefu chefu katika mimba

Tumbo iliyo njaa huenda ikafanya kichefu chefu kiwe kibaya zaidi, kwa hivyo, hakikisha kuwa unakula chakula chako mapema, na kwa wakati unaofaa. Pia, unashauriwa kuepuka kula chakula kingi, ambacho kinaweza fanya tumbo kuhisi imejaa wakati wote. Badala yake, kula chakula kidogo, mara kwa mara.

Kula pole pole na uchukue muda wako kutafuna chakula chako.

 • Chagua chakula chako vizuri

Epuka kula chakula ama harufu ambazo zinaweza kufanya uhisi mgonjwa. Pia, epuka kula vyakula vyenye mafuta, ufuta na pili pili.

Chagua chakula kilicho na kiwango cha juu cha protini na wanga, kiwango kidogo cha ufuta na ni rahisi kuchakata. Mandizi, wali, mkate, tufaha na crackers ni hiari nzuri.

Chakula chenye chumvi pia kinaweza saidia na vyakula vyenye tangawizi.

 • Lala na upumzike vya kutosha

umuhimu wa usingizi kwa afya

Uchovu unaweza fanya kichefu chefu chako kizidi. Lenga kupata angalau masaa manane ya usingizi kila usiku. Na vyema zaidi kama unaweza sinzia kwa dakika chache kila siku.

Epuka kukimbilia na kutoka kitandani mapema sana.

 • Usiwe na fikira nyingi

Fikira nyingi zinaweza fanya ishara zako ziwe mbaya zaidi. Ikiwa unahisi una kwazwa kimazo, jaribu kupunguza kazi unazo fanya. Chukua muda upumzike na upunguze fikira zako.

 • Usivute sigara, kaa mbali na watu wanao vuta sigara ama moshi ya sigara

Mbali na kuongeza nafasi zako za kuhisi kichefu chefu, kuvuta sigara katika mimba kuna athiri afya yako na ya mtoto, kabla, katika na baada ya kuzaliwa kwake.

Kuvuta sigara kunaweza sababisha mtoto kuzaliwa kama hajakomaa na baadhi ya matatizo ya kuzaliwa. Pia ni mojawapo ya ishara zinazo sababisha kifo cha ghafla katika watoto (SIDS).

Pia ni sawa kwa wamama wanao pumua hewa iliyo na moshi hata kama hawakuvuta sigara. Wana nafasi zaidi za mtoto kufa kabla ya kujifungua, mtoto mwenye uzani wa chini, aliye na matatizo ya kimwili na mengine ya kiafya.

 • Pumua hewa safi

Hakikisha kuwa chumba chako kina hewa tosha. Tafuta wakati wa kutembea nje ya nyumba. Kutembea ni aina nzuri ya mazoezi na ni nzuri kwa mzunguko wa damu mwilini.

 • Jaribu matibabu haya asili

Jaribu kunywa vinywaji vyenye tangawizi. Unaweza changanya vipande vichache vya tangawizi kutengeneza chai ya tangawizi isiyo na kafeini na ni salama kunywa. Mumunya switi za nishati ama peppermint. Ni njia nzuri ya kuwa na harufu inayo pendeza ya mdomo na kutupilia hisia za kutapika.

Wamama wengi wenye mimba mara nyingi hutamani chakula chenye ugwadu, na huenda ikawa ni sababu kwa nini kina punguza kichefu chefu. Mbali na matunda ya citric kama vile machungwa, ndimu, berries na kadhalika, unaweza jaribu kula chakula kilicho hifadhiwa kama vile pickles na jam.

 • Vitamini B6 inaweza saidia

Kiwango kidogo cha vitamini B6 kimeonyeshwa kupunguza ishara za ugonjwa wa asubuhi katika baadhi ya wagonjwa.

Wanasayansi bado hawaja dhibitisha jinsi hasa B6 huwa na athari kwa kichefu chefu, lakini huenda ika husika na jinsi inavyo chakata amino acids na kusaidia kupunguza neurotransmitters. Pia ina himiza utoaji wa seli nyekundu ambazo ni muhimu kwa afya ya mtoto.

Mayai, nyama, nafaka nzima na njugu ni baadhi ya vyakula ambavyo vina wingi wa vitamini B6. Unaweza chukua vitamini hii kama tembe.

Kumbuka kuwa, viwango vya juu vya vitamini B6 ni hatari kwa mtoto wako. Kwa hivyo, usichukue zaidi ya miligramu 200 kwa siku. Wakati wote, hakikisha kuwa unawasiliana na daktari kabla ya kuchukua tembe zozote katika ujauzito.

Matibabu Ya Kichefu Chefu: Wakati wa kumwona daktari

Mama, kumbuka kuwasiliana na daktari bila kukawia uki:

 • Una mkojo wenye rangi nyeusi ama hauja enda msalani kwa zaidi ya masaa manane
 • Una tatizika kuweka chakula ama maji kwa masaa 24
 • Hauna nguvu, kuhisi kizungu zungu unapo simama
 • Una umwa na tumbo
 • Hisi uchungu ama kutoa damu unapo kojoa
 • Umepoteza uzito wa mwili

Huenda hizi zikawa ni ishara za kukosa maji tosha mwilini ama maambukizi ya mkojo.

Vyanzo: NHS, MayoClinic

Soma PiaMatatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

Written by

Risper Nyakio