Hapa Kuna Baadhi Ya Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kutibu Kiungulia

Hapa Kuna Baadhi Ya Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kutibu Kiungulia

Wakati ambapo baadhi ya matibabu ya kinyumbani yanaweza punguza kiungulia, ikizidi, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako.

Kiungulia sio hali ya kufurahisha ya kushuhudia. Kama jina linavyo dokeza, kiungulia ni kuhisi kana kwamba una chomeka kwenye kifua na koo yako na huenda ukapata kwikwi. Kiungulia kina weza dumu kwa masaa mengi na kisipo tatuliwa, kubadilika kuwa GERD, ama maradhi ya gastroesophageal reflux. Kiungulia kinaweza sababishwa na kula chakula kingi chenye mafuta mengi ama vyakula vya asidi. Bahati ni kuwa kuna matibabu ya kinyumbani ya kiungulia.

Kiungulia ni nini?

what is a heartburn

Ukihisi kana kwamba unachomeka kwa kasi, sawa na unapo wekelewa pedi moto kwenye mfupa ya titi, una shuhudia kiungulia.

Matibabu ya kinyumbani ya kiungulia

Hapa chini kuna baadhi ya mbinu za kinyumbani ambazo unaweza tumia kutatua hali ya kiungulia.

  • Legeza mavazi yako

Kiungulia hufanyika vitu vilivyo tumboni vinapo songa kwenye oesophagus ambapo asidi ya tumbo inaweza choma kuta ya pipu ya chakula.

Kuna visa vya viungulia ambavyo vinaweza kutendekea kwa sababu unavalia mavazi yanayo kubana kwa sana na kukaza tumbo yako. Mavazi kama vile mshipi, suruali ama sketi. Kwa hivyo jambo la kwanza kufanya ni kulegeza mavazi yanayo kubana karibu na tumbo yako.

  • Simama wima

Jinsi unasimama inaweza kuwa sababu kwa nini una shuhudia kiungulia. Unapo anza kuhisi kiungulia, simama ikiwa umekaa chini na kama umesimama badilisha jinsi ulivyo simama na usimame wima.

Oesophagal sphincter ya chini huwa misuli yenye umbo la pete inayo zuia asidi tumboni kuto panda kwenye oesophagus. Kwa hivyo kusimama vyema kuna punguza shinikizo kwenye oesophagal sphincter.

  • Inua mwili wako wa juu

Kiungulia mara nyingi hushuhudiwa baada ya kula chakula cha jioni na kulala, kunaweza fanya kiungulia kizidi. Ikiwa bado una tatizika na kiungulia mara kwa mara, inua mwili wako wa juu kidogo.

Kuinua mwili wako wa juu hakumaanishi kujiinua kwa kutumia mto. Hiyo haitoshi. Lengo ni kuinua mwili wako wa juu wote. Unaweza timiza lengo hili kwa kutumia kitanda kinacho weza kuinuliwa hadi ustarehe. Lakini ikiwa hauna kitanda hiki, unaweza tumia mto wa wedge.

  • Tangawizi

Hapa Kuna Baadhi Ya Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kutibu Kiungulia

Jaribu kuongeza tangawizi iliyo siagwa ama kukata katwa kwenye supu ama chakula unacho kipenda. Tangawizi imesifika kwa muda mrefu kuwa matibabu ya kiungulia na kichefu chefu. Unaweza tengeneza chai ya tangawizi.

  • Kunywa maji yenye baking soda

Baking soda inapatikana kwa urahisi kwenye soko na maduka makubwa. Kuongeza kijiko kimoja kwenye maji yako kunaweza saidia kupunguza asidi kwenye tumbo yako. Ila, kuwa makini kunywa pole pole.

Wakati ambapo baadhi ya matibabu ya kinyumbani yanaweza punguza kiungulia, ikizidi, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako. Daktari atakushauri matibabu yatakayo kufaa.

Vyanzo: WebMd

Soma Pia:Hakikisha Kuwa Sahani Ya Mlo Ya Mama Mwenye Mimba Ina Chakula Hiki!

Written by

Risper Nyakio